Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kutokana na kupanda kwa gharama ya mbolea ya kupandia DAP na kukuzia UREA hapa nchini iliyosababishwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa Corona duniani.
Mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini (TFRA) imetoa wito kwa wakulima kutumia mbolea mbadala ikiwemo NPC pamoja NPC ZINK zinazouzwa kwa bei naafuu huku uwezo wake wa kufanya kazi unatajwa kufanana na DAP au kuzidiana.
Wito huo umetolewa na Stephan Eliuth Ngailo ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania alipokuwa mkoani Njombe kwa lengo la kufanya tathmini ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
“Hizi mbolea zinauzwa kwa bei naafuu lakini uwezo wake zinaweza zikafanya vizuri zaidi ya DAP au sawa na DAP nimeuliza gahalama kwa mkoa wa Dar es salaam zinauzwa elfu 61 na hapa ni elfu 64.Na hii NPS ZINK ambayo ina virubish vinne nimeona inauzwa kwa shilingi elfu 68 hapa Njombe kwa hiyo mkulima akishindwa kununua DAP basi aweze kununua hii mbolea ya NPS”Alisema Ngailo
Vile vile ameongeza kuwa “kuna mwenzetu pia mzalishaji wa ndani wa kampuni ya Minjingu naye tumemsisitiza kuleta mbolea zake za kupandia na kukuzia kwasababu nazo zina bei naafuu,kuna mbolea zingine ambazo zinasambazwa na kampuni ya YARA zinaitwa YARA mira kuna otesha pia kwa hiyo mkulima anaelimishwa kuwa na uwanja mkubwa wa kuweza kuchagua kwa hiyo na sisi tupo ili kuchagiza hiyo.Kwa UREA unaweza ukatumia CAN au SA zenye bei naafuu kwa hiyo mkulima ana uwanja mkubwa” Alisema Ngailo
Katika hatua nyingine bwana Ngailo amesema licha ya kupanda kwa bei ya mbolea katika soko la dunia lakini upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya nyanda za juu kusini unaridhisha.
“Upatikanaji wa mbolea unaridhisha kwa kiasi kikubwa,katika mikoa yote mitatu tuna tani zaidi ya elfu nane.Mbinga kuna zaidi ya tani elfu moja,Ruvuma kuna zaidi ya tani elfu mbili,na hapa Njombe kuna zaidi ya tani elfu tano.Na kwa bahati nzuri hawa wanaosambaza mbolea wametueleza bado kuna mbolea inakuja”alisema Ngailo
Kwa upande wake Sad Mwang’onda meneja wa kampuni ya Mtewele General Traders ambao ni wasambazaji wa mbolea mkoani Njombe amewahikishia wakulima upatikanaji wa mbolea wakati wote.
“Tutaendelea kuhakikisha pembejeo zinakuwa karibu na wakulima na kama mnavoona sasa hivi tunajiandaa na msimu wa kilimo lakini maghala yetu yana mbolea ya kutosha na nyingine bado iko barabarani inakuja na tutaendelea kuhakikisha mkulima hapati changamoto kwenye upatikanaji wa mbolea na pia tutajitahidi kuhakisha bei kutokuwa ya kumuumiza mkulima”alisema Sad Mwang’onda
Stephan Eliuth Ngailo mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) akiwaeleza waandishi wa habari hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini pamoja na kutoa wito kwa wakulima kutumia mbolea mbadala zenye bei naafuu sokoni. Baadhi ya mbolea zilizopo kwenye moja ya ghala la msambazaji wa mbolea mkoani Njombe Mtewele General Traders zikionekana wakati mkurugenzi wa TFRA alipofika mkoani humo kukagua upatikanaji wa mbolea.APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments