Charles James, Michuzi TV
WANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College) wameishukuru Serikali kwa namna inavyofanya maboresho makubwa kwenye Chuo hicho ambayo wanaamini yatasaidia kukuza taaluma zao.
Wametoa kauli hiyo chuoni wakati wakizungumza na wandishi wa habari ambapo wamesema ujenzi wa mabweni ndani ya eneo la chuo utawarahisishia kuwahi vipindi tofauti na mwanzo ambapo wengi wao walikua wanaishi mtaani na hivyo kukutana na changamoto ya usafiri.
Akizungumzia maboresho hayo Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Wema Justine amesema ujenzi wa mabweni hayo yatakayokua na uwezo wa kubeba wanafunzi 420 utawarahisishia kuwahi vipindi kwa haraka kwani watakua wanaishi ndani ya Chuo na hivyo kuondoa adha ya usafiri waliyokua wanakutana nayo.
"Niipongeze Serikali yetu kupitia Wizara ya Elimu kwa kutufanyia maboresho haya kwenye Chuo chetu, kwetu sisi ni Ujumbe kwamba serikali yetu ni sikivu na inalenga kutuekea sisi wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia ili tuweze kukuza kiwango chetu cha ufaulu.
Uwepo wa mabweni haya kwetu ni faida maana tumekua tukipata changamoto ya usafiri wa daladala na wakati mwingine kulazimika kutumia kiasi kikubwa cha fedha kupanda bodaboda ili tuwahi vipindi lakini sasa tutaishi ndani ya Chuo," Amesema Wema.
Kuhusiana na kusoma masomo ya umeme anasema ndoto zake zilikuwa kuja kuwa Mhandisi hivyo alivyofika chuoni hapo na msukumo wake ulikuwa katika masomo ya Sayansi alimua kujiunga na kozi ya umeme.
“Mimi nilikuwa napenda umeme na nilivyokuja hapa chuo nikakutana na Biometical nikaelezewa jinsi ilivyo na walionitangulia nikaipenda nikaamua kuingia kwenye Biometical,” Amesema.
Nae Innocent Michael Mwanafunzi wa Diploma amesema maboresho hayo yamelenga hadi katika vifaa vya kufundishia na wao kama wanafunzi wa kozi za uhandisi wamenufaika pia.
"Sisi ambao tunasoma kozi za uhandisi tumeletewa baadhi ya vifaa vipya vya kujifunzia na hivyo kuturahisishia pale tunapokua tunajifunza kwa vitendo, mathalani hapa tumeongezewa vifaa na ndio kama hivi mnatuona tuko kwenye kutengeneza mashine za kutotolea vifaranga," Amesema.
Muonekano wa Bweni la Wasichana katika Chuo cha Ufundi Arusha pindi litakapokamilika.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments