Moshi. Ni Mshangao na maajabu ya aina yake yaliyoambatana na simanzi na vilio pale wanandoa wawili waliozaliwa siku moja, mwaka mmoja na kufariki siku moja ambapo wamezikwa leo kwa pamoja katika kata ya Rau, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Wanandoa hao ambao ni Kundaeli na Monyiaichi Kimaro ambao walipishana masaa machache ya vifo vyao Julai 29 mwaka huu walizaliwa mwaka 1946.
Pamoja na kuzaliwa siku moja pia wanandoa hao walibatizwa na kubarikiwa siku moja katika kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT),Mwika Kati mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Agosti 2 mtoto wa familia hiyo, James Mbando amesema hata wakati vifo hivyo vinatokea hakuna hata mmoja aliyeshuhudia kifo cha mwenzake.
"Kifo hiki kimetuumiza kama familia kuwapoteza wapendwa wetu kwa wakati mmoja maana hata wakati baba na mama wanafariki hakuna hata mmoja ambaye alijua kifo cha mwenzake,"amesema
"Mama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na hata alipozidiwa alikimbilia hospitali ya Mawenzi huku wakati huo na baba naye akikimbilia hospitali ya KCMC kwa hiyo kila mtu alikufa kwa wakati wake lakini wakipishana masaa machache,"amesema James
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments