WASANII, WANAHABARI NA WANAMICHEZO KUPATIWA CHANJO JIJINI DAR | ZamotoHabari.

Na John Mapepele

WIZARA  ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeratibu zoezi la hiari kwa wadau wa sekta hizo kupatiwa chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi, ameeleza kuwa makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli kwamba kwa mazingira ya  kazi zao, wako katika hatari ya kuambukizwa.

“Shime kwao kujitokeza siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi kwa hiari yao wale waliojiandikisha katika Mabaraza na Idara zao husika,” amesema Dkt. Abbasi.

Aidha, amesema kwa wale waliokosa kujiandikisha awali wawe Wasanii au Wanahabari au Wanamichezo wajiandikishe mapema kupitia namba 0654063274 au barua pepe matiko.mniko@basata.go.tz  ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Amefafanua kuwa Wasanii walio nje ya Dar es Salaam wataendelea kutumia utaratibu unaoendelea kutangazwa na Wizara ya Afya.

Ametoa mwito kwa Wasanii, Wanahabari na Wachezaji kwa hiari yao kujitokeza na kutumia fursa  hii kipata chanjo ili kujikinga na kuwakinga wengine na ugonjwa wa UVIKO 19.


 Katibu Mkuu wa  Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akipata chanjo katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam hivi karibuni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuizindua rasmi kitaifa



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini