Na.Khadija Seif, Michuzi TV
TAASISI ya Happy Hands imesema fedha zitakazopatika katika tamasha la Msanii Maher Zain kutokea Sweden mwenye asili ya Lebanon, watazikabidhi kwa Watu Wenye Ulemavu wa kuona.
Tamasha litafanyika Machi 12 mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kwa kushirikisha nyota wa Muziki wa bongo fleva, Ali kiba na Suma lee.
Muandaji wa Tamasha hilo, Zainab Ally amesema Tamasha hilo mahususi kwa kwa ajili ya kutangaza utalii wa ndani.
Alisema fedha zitakazopatika katika tamasha hilo litapelekwa katika Jumuiya ya Maendeleo ya Waislamu Wasiona Tanzania (VIMDAT) ili kusaidia mambo mbalimbali katika jumuiya hiyo.
"Fedha zitakazopatika zitaelekezwa katika kwa watu walemavu wasiiona, pia tunatagemea Maher alikja kutembelea katika vivutio vya utalii vya Arusha na Ngorongoro andapo akiwa na muda, " alisema.
Rais wa Jumuiya ya Maendeleo ya Waislam Wasiona Tanzania (VIMDAT), Salim Benedicto alisema anashukuru Taasisi hiyo kwa kuwaangalia jumuiya hiyo na Kuonyesha Nia ya kutaka kuwasaidia na ni jambo nzuri kuona jamii inasaidia na kuwajali watu wenye ulemavu ambapo ni faraja kwao.
"Tunashukuru kusikia fedha zitakazopatika katika tamasha hili zitaelekezwa katika jumuiya yetu, " alisema Benedicto.
Muakilishi wa Msanii Ali Kiba, Mwijaku ametoa wito kwa waislamu na watanzania wote kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji.
Amesema kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji ni ibada na kufanikiwa kwa mambo mengine ambayo unayafanya.
Muandaji wa Tamasha la Msanii Maher Zein, Zainab Ally linalotarajiwa kufanyika Machi 12 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es salaam ambapo Msanii Alikiba ni Miongoni mwa Wasanii watakaotoa burudani.
Mwakilishi wa Lebo ya King's Music Mwijaku akitolea ufafanuzi fursa Kwa Wasanii ambayo wamepatiwa kutoa burudani jukwaa Moja na Msanii wa Kimataifa Mahir zein kutoka SwedenTembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments