MAMA SAMIA AONGEZA BILIONI 1 MFUKO WA MAENDELEO WA SANAA NA UTAMADUNI | ZamotoHabari


Na.Khadija Seif, Michuzi TV

WAZIRI wa Utamaduni,Sanaa na Michezo ameweka wazi kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu ana dhamira ya kuboresha na kunyanyua kazi za Sanaa nchini kwa kuongeza Fedha Kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni.

Akizungumza na wadau wa kazi za Sanaa nchini Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania inatambua Mchango wa kazi za Sanaa nchini na awamu ya 6 imedhamiria kuboresha Miundombinu ya kazi za Sanaa na Kwa kuanza ameweka billion 1 Kwa Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni.

"Dhamira yangu ni kuona Sekta ninazo simamia kuona zinapiga hatua kubwa tunahitaji kufanya Mapinduzi nakuona Maendeleo ya Sanaa ya Filamu nchini hivyo Serikali Ina dhamira pia ya  kuhakikisha kazi za Sanaa zinafika mbali na zinakuwa zenye viwango na Mama Samia ameongeza takribani bilioni 1 na kufikia bilioni 2.5 katika Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa hivyo Wasanii wajitokeze kukopa Fedha hizo ."

Hata hivyo Mchengerwa ameeleza kuwa Wasanii Wizara itahakikisha wanachapa kazi na hakuna kazi ya Sanaa itakayosimama Kwa kisingizio cha Fedha kwani Milango ipo wazi Kwa wadau wa Filamu kukopesheka Kwa Fedha hizo Ili kuona Kwa namna gani watayarishaji wanatengeneza kazi zenye viwango na Bora zenye kutambulisha Utamaduni wa Taifa la Tanzania.

"Ule mkamwo wa kusitasita kutengeneza Filamu zenye uhalisia Sasa basi tayari Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa una shilingi Bilioni 2.5 ni Fedha Kwa ajili ya kazi za Sanaa ambapo Mtayarishaji atakopeshwa Fedha hizo bila malipo ya riba hivyo tunategemea kazi za Sanaa nzuri zitazalishwa Kwa wingi na zenye ubora Ili kufikia Masoko ya nje."

Aidha, Mchengerwa ameeleza dhamira nyingine ya wizara yake kuweka Mkakati wa wizara kuwa na televisheni na radio Ili kuweza kuonyesha kazi za Sanaa Kwa masaa 24 na kuwapa fursa Wasanii wanaochipukia kuonekana Pamoja Mkakati wa wizara kuwa na Vyombo vya kisasa vya kuandaa Filamu ambavyo vitakuwa vikikodishwa .
 
Pia Waziri huyo amewaomba Wasanii kuonyesha ushirikiano na wizara husika na kuahidi kushikamana na wasanii  bega Kwa bega na Wasanii kuhakikisha kazi zinajitangaza na kuwaleta watu wenye Mchango katika Sekta ya Filamu kidunia Ili kusaidia kiwanda cha Filamu nchini kinakua na wigo mpana .                                                      
Mchengerwa ameongeza kuwa Wizara Ina Mkakati wa kujenga nyumba Kwa Wasanii zenye hadhi kwani Serikali inatambua Mchango wa Sanaa nchini katika kutangaza Utamaduni.  
           
Kwa upande wake Katibu Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo amebainisha changamoto na Mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia vikao vilivo fanyika Kwa kushirikisha viongozi,Wasanii na wadau wa Filamu na vyama vya Wasanii.

"Katika Mafanikio yaliyopatikana kupitia Serikali ya Jamhuri wa Tanzania Kwa kushirikiana na bodi ya Filamu nchini tuliweza kushirikisha vyama vya Wasanii , Wasanii na wadau na tukagundua vitu mbalimbali ikiwemo swala la kupatiwa Tuzo kama kielelezo Cha kutambua Mchango wa kazi za Sanaa na 2021 tuliweza kufanikiwa kuwepo Kwa Tuzo za Sanaa".

Aidha Kiagho ameongeza kuwa mbali na kuwepo Kwa Tuzo kulihitajika Mitaji Kwa ajili ya kuongeza ubora wa kazi zao pamoja na changamoto ya Kodi na tozo Kwa Filamu.

Pia  amebainisha baadhi ya Mafanikio yaliyopatikana ikiwemo Filamu mbili "Vuta nikuvute" na Filamu ya "Binti" kushinda Tuzo pamoja na Kuonyeshwa katika Mtandao wa Kimataifa wa kuonyesha Filamu Netflix.

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa akizungumza na wadau wa tasnia ya Filamu  mara baada ya kufanya kikao nao na akiwasilisha dhamira ya dhati ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kazi za Sanaa zinafanyika katika viwango vinavotakikana na kuweka bayana kuwa takribani shilingi  bilioni 2.5  zimetolewa Kwa akili ya wasanii kukopeshwa
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Dkt. kiagho Kilonzo akifafanua zaidi katika kikao Mkakati kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa JNICC Jijini Dar es salaam na kueleza Mafanikio na changamoto zilizoweza kuwasilishwa katika vikao vya ndani vilivoweza kutolewa na Wadau,Wasanii  na Watayarishaji wa Filamu nchini
Msanii wa Filamu na Bongofleva  Doki wenslaus akiwa ni Mmoja ya wasanii waliohudhuria kikao cha wadau wa Filamu kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa JNICC Jijini Dar es salaam
 
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini