Meridianbet Mkuchu Cup Inavyoendelea Kubamba Kunduchi! | ZamotoHabari

 

*Hii Ndio Nyumba Ya Mabingwa! 

SOKA la kitaa linaendelea kuwa fursa kwa vijana na chachu ya ushirikiano. Meridianbet Mkuchu Cup imechukua taswira hii kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya kata ya Kunduchi na sehemu mbalimbali za Dar es salaam.

Meridianbet Mkuchu Cup ilianza kwa kushirikisha jumla ya timu 20 kutoka maeneo ya Mwananyamala, Mwenge, Kinondoni, Magomeni, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Kawe, Mabwepande na Msasani katika dimba la Machava.

Lengo la michuano hii ambayo imemaliza ngazi ya robo fainali wikiendi iliyopita, ilikuwa ni kutoa fursa kwa vijana kuweza kuonesha vipaji vyao. Pia, michuano ya Meridianbet Mkuchu Cup ilikuwa ni fursa ya vijana kupata ajira kwa kulipwa kuziwakilisha timu zinazoshiriki, na ilikuwa fursa ya kuwakutanisha vijana na kuchochea umoja baina yao.

 "Vijana ni nguvu kazi ya taifa, na wana vipaji sana lakini baadhi yao bado hawajaonekana vyema kwenye tasnia ya soka, michuano hii inawapa nafasi ya kuonekana kwa jamii na kujipatia fursa ya ajira. Pia, hii ni burudani kwa wananchi wanaohudhuria michuano hii." Alizungumza Emmanuel Mkuchu, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kilongawima, ambaye ni mratibu wa michuano hii kwa kushirikiana na Meridianbet.

Wikiendi hii mechi za robo fainali za ligi ya Meridianbet Mkuchu Cup zimemalizika na kutoa washindi wanaosonga hatua inayofuata. Kwenye robo fainali, Mabwe Young Boys waliwachakaza Mtongani Family goli 3 - 0, huku Nondo FC wakiwachapa Kilongawima Boys 2 - 0, wakiungana na Tanga Boys pamoja na Mianzini ya Magomeni kuelekea Nusu Fainali.

Kwa upande wa Meridianbet, ambao ni wadhamini wa michuano hii kupitia Twaha Mohamed, anayetokea kitengo cha masoko cha kampuni hii wanasema, hii ni sehemu yao ya shughuli ya kurejesha kwa jamii na kutoa fursa kwa vijana.

"Vijana wanaonesha uwezo mkubwa sana hapa, sisi kwetu huu ni muendelezo wa jitihada zetu za kushirikiana na jamii, tukiwa tunarejesha kwa jamii tunayoshirikiana nayo kila siku."

Nusu fainali ya michuano hii inayotarajiwa inatarajiwa kuchezwa Februari 11 na 12 na kurudiwa tarehe 18 na 19 na kisha fainali ikipangwa kuchezwa Februari 26. Bila shaka ungependa kujionea burudani ya soka na vipaji kutoka mtaani kupitia Meridianbet Mkuchu Cup.

Meridianbet pekee, mabingwa ndiyo nyumbani kwao!



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini