Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka wasanii wanaopanda leo Februari 24,2022 kuiwakilisha Tanzania kwenye Maonesho makubwa ya kimataifa ya Dubai Expo, Mfalme wa Singeli Sholo Mwamba na Mkongwe wa Muziki wa Asili wa Tanzania Mrisho Mpoto kuendelea kutoa burudani ya kukata na shoka ili kuitangaza Tanzania kimataifa.
Mhe. Mchengerwa amesema haya leo Februari 24,2022 wakati ambapo Sholo Mwamba anatarajia kuendelea kuwaipagawisha dunia kwa nyimbi za singeli majira ya saa 11:00 jioni kwenye ukumbi wa Earth Stage baada ya kufanya vizuri kwenye onesho lake la awali Februari 22, 2022 na kuwaacha umati uiliofika kucheza naye huku wengine wakichukua picha kwa ajili ya matumizi yao.
“Tunataka Singeli na muziki wa kwetu uiteke dunia ambapo kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeanza vizuri safari ya mapinduzi makubwa ya sanaa kwenye anga za kimataifa” amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Naye Msanii Mpoto anatarajia kufunga kazi katika ukumbi huo kwa kuendeleza shoo kali baadaa ya kukonga nyoyo za wageni katika mitaa ya jiji la Dubai.
Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Falme za Kiarabu Mhe. Mohamed Mtonga leo Februari 24, 2022 amewapokea wasanii mbalimbali kutoka Tanzania wakiwa na lengo moja tu la kuitangaza Tanzania ili kuvutia wageni kutembelea hatimaye kuliingizia taiafa mapato.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Sholo Mwamba na Mrisho Mpoto wameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa hiyo adhimu ya kuutangaza utamaduni wa Tanzania kupitia sanaa ili kuitangaza Tanzania.
“Leo ndiyo leo, tunakwenda kukamilisha kazi tuliyotumwa na taifa letu, kwa kuutambulisha utamaduni wetu na kuwakaribisha wageni kuja Tanzania. “amesisitiza Mpoto.
Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amesema wageni kutoka mataifa mbalimbali wameyapokea vizuri maonesho ya wasanii kutoka Tanzania hivyo ni mategemeo kwamba kutakuwa na matokeo chanya katika malengo ya maonesho haya.
Kikosi cha wasanii wa Tanzania kwenye Dubai expo kikiongozwa na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchi za Falme za Kiarabu Mhe, Mohamed Mtonga( aliyevaa kitambulisho)
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments