Njombe mji Fc yaamka upya,viongozi wa mpito macho yao ni ligi kuu | ZamotoHabari



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Uongozi wa mpito wa Club Njombe inayoshiriki ligi daraja la pili umefunguka mazito katika kuiongoza ligi hiyo ili iweze kurejea ligi daraja la kwanza (Champion ship) na hatimaye ligi kuu.

Katibu mkuu wa Club ya Njombe mji bwana Johnson Mgimba amewaeleza wanasoka kuwa Club hiyo imepata uongozi wa mpito hivi karibuni na kuweka malengo makubwa ya kuhakikisha Club hiyo inarejea daraja la kwanza mpaka ligi kuu ili kuendelea kuwaletea burudani wapenda soka wa mkoa wa Njombe.

“Ukianguka unatakiwa usibaki hapo hapo,inatakiwa usimame na kusonga mbele,na sisi viongozi wa mpito tumedhamiria kwa dhati kuhakikisha tunatekeleza matakwa ya wananjombe ya kuona timu yetu ya Njombe mji tunaitengenezea njia ili iweze kurudi ligi kuu”alisema Mgimba

Katibu ameomba ushirikiano kwa wananchi wa mkoa wa Njombe ili kutekeleza dhamira yao ya kuiboresha timu.

“Wadau wote wa Njombe mji tunakualika utoe mawazo yako katika kuijenga Njombe mji na sisi viongozi wenu tunataka mawazo ili kuiletea mawzo timu yetu”aliongeza Johnson

Vile vile amesema timu inaanza kuingia kambini ili iweze kumalizia michezo yake katika duru ya pili inayoanza jumamosi

“Tumeshaiandaa bajeti yetu ili tuweze kumaliza hii mizunguko yake sita,tunawashukuru sana wadau wote kwa michango yenu kwa kuwa tuna kila sababu ya kuirudisha timu yetu katika ligi kuu na kuomba wadau kuendelea kujitoa kwa ajili ya timu hiyo”anasema Mgimba

Aidha katibu amemshukuru Dokta Thobias Lingala ngala ambaye ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Njorefa kwa kusaidia ukarabati wa hostel zilizopo sabasaba kwa ajili ya kuwaweka pamoja wachezaji.

Viongozi wa mpito wa club hiyo waliochaguliwa hivi karibuni ni Stiven Njowoka mwenyekiti wa Club,Hamidu Ngole makamu mwenyekiti,Johnson Mgimba katibu mkuu,Alex Mhagama naibu katibu mkuu,Elizabeth Kilindi mhazina,Japhari Mgenda mjumbe,Maulid Ngole mjumbe,Vasco Simbaya mjumbe na Monlee Samsoni akiwa ni afisa habari wa Club hiyo.


 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini