SIMBA SC YAONDOKA NA ALAMA TATU MBELE YA ASEC MIMOSAS | ZamotoHabari



Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC wameanza vyema hatua ya makundi ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) baada ya ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast kwenye mchezo uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba SC ilianza kupata ushindi huo dakika ya 12 ya mchezo kwa bao safi la Mshambuliaji Pape Ousmane Sakho aliyepiga ‘Acrobatic Kick’ safi iliyojaa wavuni na kumuacha Golikipa wa Asec, Yao Attohoula akiwa hana la kufanya, bao hilo la Simba SC lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinaisha.

Asec Mimosas walirejea kipindi cha pili kwa kasi, iliyozaa bao la kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Mchezaji wake, Aziz KI baada ya kuichambua safi ngome ya ulinzi ya Simba SC iliyokuwa ikiongozwa na Henock Baka na Joash Onyango.

Kipindi hiko hiko cha pili, Simba SC alikuwa kama amejeruhiwa, baada ya kuingia Nahodha John Bocco na Yusuph Mhilu ambao walileta ahueni kubwa na kupelekea kupata mkwaju wa Penalti dakika ya 79 na Penalti hiyo ilikwamishwa kambani na Beki Shomari Kapombe.

Bao la tatu na la mwisho lilifungwa na Mshambuliaji Peter Banda dakika ya 81 baada ya John Bocco kupiga krosi safi iliyotokea upande wa kushoto upande wa lango Asec Mimosas.

Simba SC ipo Kundi D kwenye Michuano hiyo ya CAF CC sambamba na timu za Asec Mimosas ya Ivory Coast, RS Berkane ya Morocco na US Gendermarie ya Niger.







Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini