Bahati Bendi yatoa shangwe la kutosha tamasha la kuchangia Twiga Stars | ZamotoHabari


Historia imeandikwa usiku wa leo, Machi 8, 2022 kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuadhimisha siku ya mwanamke duniani kwa kufanya changizo kwa ajili ya kuinua michezo ya wanawake kupitia Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars.

Sherehe imeanza kwa kupambwa na wasanii wa kike kutoka bendi ya muziki ya wanawake ya Bahati.

Aidha, kikosi cha kutoa hamasa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kimetoa burudani ya aina yake kwa kuwapokea wageni wote kwa burudani ya matarumbeta na ngoma.

Wadau mbalimbali wameshiriki kwenye sherehe hii ya kuchangia Twiga Stars.

Sherehe hii pia imeratibiwa na Wizara kwa kushirikiana na taasisi ya Dadahood ambayo imezindua albamu ya nyimbo ya Orange.























Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini