Dina Marios na siku ya Wanawake Duniani!

Nataka nikwambie kitu wewe mwanamke mwenzangu tena Sitakwambia maneno mengi.
La Kwanza na la msingi Kuwa na hofu ya Mungu,Mtegemee Mungu kwenye Kila kitu.Kuwa Na Imani kubwa na Mungu wako.Moyo wako uwe na Shukrani na Subra na Akili yenye Utulivu.

La Pili ....JIAMINI,JIKUBALI,JIPENDE!
Ukifanikiwa kwenye haya my dear hakuna kitakachokuyumbisha wala kukuogopesha.Haijalishi Size ya Mwili wako Mnene au mwembamba,Mfupi au mrefu,mweusi au mweupe....JIAMINI,JIKUBALI na UJIPENDE.
.
La Nne...Kuwa na Visions/Maono
Kuwa Na jambo linalokutambulisha iwe ni kazi au biashara au harakati.Na hakikisha una maono Nayo sio unadandia maono ya watu.Sisi wengine Tupo deep sana tunaweza kulala Usingizini Na tukapata maono ndotoni ya jambo fulani.Nikalifanya Na likakubalika Basi na wewe umo ushaiga.
Kuwa Na Ndoto kubwa..maono makubwa kulingana na Namna Umetambua Kusudi Lako hapa duniani.
.
La Tatu pamoja na majukumu yote,kazi zote na harakati zote hakikisha unajipa muda ya kufurahi Na kuburudika..Majukumu usiache yakakuzeesha.Na kukunyima kafursa ka kukunjua mwili,nafsi Na Sura.
.
Ushindi Pamoja...
Kama Kuna wanawake unaweza kushirikiana nao kwenye mambo mbali mbali ya kiuchumi,malezi,mapishi,Ibada,kusoma vitabu,burudani,michezo,Fursa mbali mbali basi Ungana nao kuweza Kushinda nao.
Wanawake wanapoungana Mambo Makubwa Hutokea...Ushindi Pamoja.
.
Happy Women’s Day Kwa wanawake wote wa Shoka!
Dina Marios!

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini