MKALI WA JIKO YAONGEZA MIKOA YAKUSHIRIKI | ZamotoHabari

 Na.Khadija Seif, Michuzi TV

MSIMU wa tatu wa Mkali wa jiko wazinduliwa rasmi jijini Dar es salaam wanawake watakiwa kuchangamkia fursa hiyo katika Sekta ya Upishi.

Akizungumza na Waandishi Wahabari Muandaaji wa Shindano hilo Zainab Issa amesema Msimu huu utakua watofauti kutokana na kuongezeka Kwa Mikoa ya kushiriki katika Shindano hilo kutokana na watu wa Mikoani kuonyesha muamko wa kuhitaji Shindano.

"Msimu huu itajumuisha Mikoa minne ikiwemo Dodoma,Tanga,Arusha pamoja na Mkoa wa Dar es salaam ."

Hata hivyo amesema sababu za Mikoa hiyo kushirikishwa kutokana na Misimu iliyopita waliweza kukusanya washiriki wengi hivyo imeleta Muamko Kwa wapishi hususani wa Majumbani kuonesha ujuzi wao Kwa Mikoa mi tatu mingine.

Aidha amewaomba Wapenzi wa kipindi hiko cha  "Mkali wa jiko" kuendelea kufatilia matangazo mbalimbali Ili kujua Mkoa husika watafika lini Kwa ajili ya usahili na Kwa zawadi ya Mshindi itakua Cheti Cha kutambua ushiriki wake,Fedha pamoja na zawadi nyingine nyingi.

pia akaongeza kuwa Kipindi hiko rasmi kitaanza   Mei 7 mwaka huu na kitarushwa Mubashara katika chaneli ya UTV .

Muandaji wa Tamasha la"Mkali wa jiko " Zainab Issa akizungumza na Waandishi Wahabari mara baada ya kuzindua rasmi Msimu wa 3 wa Shindano hilo Jijini Dar es salaam na Kuwahimiza wanawake hususani wa Majumbani kujitokeza katika usahili


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini