NANI KUONDOKA NA MILIONI 985,669,400 ZA SPORTPESA? | ZamotoHabari

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
KAPUNI  ya burudani na michezo SportPesa inapenda kuutaarifu, uma wa watanzania, wadau na wapenda michezo ya kuwa Jackpot yetu endelevu imefikia kiwango cha shillingi za millioni 985,669,400.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni hiyo, Tarimba Abbas amesema kwa sasa hakuna kampuni yoyote yenye dau kubwa zaidi ya hilo na kumtangaza mshindi wa Jackpot kubwa kama hii, ambapo mpaka sasa hii ni mara ya tatu kwa Jackpot endelevu kupanda kwa dau zaidi ya nusu bilioni, baada ya kuanzia shilingi milioni 200.
 
“Kwa hakika, kiwango hiki kama hakitapata mshindi mwishoni mwa wiki hii, basi dau litakalofuata, litaweka historia ya kuwa dau la kwanza la ubashiri kufika bilioni moja kwa viwango vya Jakipoti endelevu nchini”.
 
‘’Tunapenda kuwasisitiza watanzania wote kwa ujumla kucheza mara nyingi kadiri muwezavyo Ili kupata nafasi kubwa ya kushinda Jackpot hii nono ambayo ilianza kushindaniwa kuanzia mwezi wa 4, 2021 baada ya mshindi wa 7 wa Jackpot Abdulaziz Ngámilo kupatikana.
 

“Jambo jema ama zuri kwa wachezaji ni kwamba hata kama hukufanikiwa kushinda dau hili moja kwa moja una nafasi nyingine ya kushinda kupitia Jackpot bonasi kwa washindi wanaopatia kuanzia timu 10,11 na 12, amesema Tarimba.

Amesema tangu kuanza kwa Jackpot hii karibu miezi 11 Iliyopita, SportPesa imetoa washindi wa kitanzania zaidi ya 200 kila wiki kwa waliobashiri kwa usahihi kuanzia mechi 10, 11 na 12.
 
“Washindi wa SportPesa jackpot kwa mara ya kwanza walipatikana mwaka 2019 Agosti, ambapo Magabe Marwa na Kingsley Pascal waligawana Tsh. 825,913,8640 baada ya jackpot hii kukaa kwa miaka miwili,” ameeleza Tarimba.
 
“Kwa mara ya pili na tatu walipatikana washindi wengine ambao ni Scolastika Ngwaluweson na Jamal Khalfan Abdallah ambapo waliondoka na kiasi cha shilingi 260,319,980Tsh na 288,974,720Tsh kila mmoja.”
 
“Washindi waliofata ni Lilian Laizer na Yassini Ridhiwani ambao walijishindia 267,800,060 Tsh na 437,631,320 Tsh kila mmoja.”
 
Akiongezea kuhusiana na dau hilo na namna ya kushinda, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Sportpesa Tanzania, Sabrina Msuya amewataka watanzania kuchangamkia fursa bila kusita wala kuwa na visingizio ili kuwa mabilionea.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini