Sekta za Burudani zina Mchango Mkubwa- Mhe. Mchengerwa | ZamotoHabari


Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinatoa mchango mkubwa wa kifedha kutokana na sekta za burudani.

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Machi 25, 2022 wakati alipokuwa akiwasilisha maelezo ya rasimu ya mpango wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Amesema kutokana na utafiti uliofanywa na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PWC) katika nchi za Afrika, sekta za burudani na vyombo vya mawasiliano (Entertainment and Media (E&M), An African perspective) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2022 zinaonekana zinaendelea kwa kiwango kikubwa na zinatoa mchango mkubwa wa kifedha katika nchi hizo.

“Katika kipindi cha mwaka 2017 mapato ya ujumla kutokana na sekta za burudani na vyombo vya mawasiliano (Entertainment and Media – E&M) katika Tanzania yalifikia Dola za Marekani milioni 496 (sawa na shilingi Trilioni 1.17) ambapo yaliongezeka kwa asilimia 28.2 kutoka mwaka 2016. Kwa kuendelea ukuaji wa wastani wa asilimia 18.3 mapato hayo yanatarajiwa kufikia Dola bilioni 1.1 (sawa na shilingi Trilioni 2.59) mwaka 2022”. Amefafanua Mhe. Mchengerwa

Aidha, amesema mwaka 2018 sekta za burudani hapa nchini ilikuwa kwa asilimia 13.7 na kuongoza kwa ukuaji ambapo ilifuatiwa na sekta ya ujenzi. Mwaka 2019 ilishika nafasi ya pili kwa kukua kwa asilimia 11.2 na mwaka 2020 ilikuwa na ukuwaji hasi kwa asilimia 4.4.

Ameongeza kuwa sekta ya sanaa na burudani ikisimamiwa vizuri inamchango mkubwa kwa mawanda ya ajira, kuchangia uchumi pamoja na kukuza na kuendeleza utalii.

„Kwa ujumla Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zina umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya nchi kwa upana wake na kwa mwananchi mmoja mmoja. Pamoja na mambo mengine, Sekta hizi zina nguvu kubwa ya ushawishi, uhamasishaji na ustawishaji wa jamii na maendeleo ya nchi. Kutokana na msingi na umuhimu wake huo, Sekta hizi zinafahamika kama Nguvu Laini (Soft Power) ya Nchi”. Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Pia amesema kwa umuhimu wake, sekta hizi zimekuwa na mvuto mkubwa kwa makundi mabalimbali ya jamii na hususan vijana ambao ndio wanaunda sehemu kubwa ya nguvu kazi ya nchi, ambap amefafanua kwamba kwa kuzingatia hali hiyo, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III) 2021/22 – 2025/26s navyo vimeelezea umuhimu wa Sekta hizi katika kuleta maendeleo makubwa ya nchi.

Mwenyekiti Kamati hiyo Stanslaus Nyongo amemshukuru Mhe. Waziri kwa ubunifu mkubwa ambapo amesema anaimani kuwa anakwenda kuleta mapinduzi makubwa ambapo ameishauri Wizara kushirikisha wadau wa sekta binafsi kwenye kuwekeza kwenye michezo.

Aidha aimeitaka Wizara kukaa jirani na wadau wa sekta hizo na kuwasilikiza ili waweze kufanya vizuri zaidi katika kukuza na kuendeleza sekta hizo.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini