SHULE YA KIMATAIFA YA KIFARANSA WAANDAA TAMASHA GOLDEN TULI ILI KUPATA FEDHA KUSAIDIA WANAFUNZI | ZamotoHabari

Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

SHULE ya Kimataifa Kifaransa iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam imeandaa 'Fashion Show' maalum itakayofanyika Machi 26 mwaka huu katika Hoteli ya Golden Tulip na zaidi ya wageni waalikwa 300 wanatarajiwa kuhudhuria siku hiyo.

Akizungumza leo Machi 15,2022 kuhusu Fashion Show inayokwenda na Kauli mbiu inayosema 'Pigania Ndoto yako' , Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Kimataita ya Kifaransa Rajab Katunda amesema tayari tiketi kwa ajili ya kuingilia kwenye tamasha hilo litakalokuwa la ubunifu zaidi zimeshaanza kuuzwa tangu Machi 1 mwaka huu katika Hoteli ya Golden Tulip-Epid'or French School.

"Tiketi zinauzwa kwa VIP kwa Mtoto ni Sh.70,000, wakubwa Sh.120,000 na tiketi za VVIP inauzwa Sh.170,000.Matarajio yetu ni kuwa na wageni waalikwa 300 na katika ya hao wamo viongozi, watu mashuhuri, mabalozi, wadau wa maendeleo, wabunifu wa kada mbalimbali na wananchi.

"Tamasha hili litajumuisha wana mitindo wengi ambao wengi wao mnawafahamu hapa Tanzania na wengine sio watanzania , na dhumuni kubwa tunataka kusaidia ushirikiano baina ya shule yetu, Ubalozi wa Ufaransa na nchi yetu Tanzania na katika hili ni tusaidia na kutoa michango kwa mashirika kadhaa yenye uhitaji.

"Pia kutakuwa na utaratibu wa kupata ufadhili wa kulipiwa ada kwa Watanzania katika shule yetu ambao hawana uwezo na siku ya tamasha hilo utaratibu huo utelezwa , lengo ni kuwapa nafasi Watanzania ambao wanataka kusoma kwenye shule yetu ambayo iko tangu mwaka 1967,"amesema.

Katunda ameongeza mpaka leo hii wanakaribia kuwa na wanafunzi 380 na kati ya hao asilimia 30 ni watanzania wanaolipa ada na asilimia 70 ni mataifa mengine.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo pamoja na mambo mengine amesema fedha ambazo wanatarajia kukusanya fedha Sh.milioni 20 ambazo zitakwenda kusaidia wanafunzi wenye uhitaji."Tunafahamu kuna watoto wenye uhitaji maalumu walioko shuleni na wanatamani kutimiza ndoto zao, hivyo lengo letu ni kusaidia jamii yenye uhitaji."

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Shirika la Child Suport Tanzania Noelah Msuya Shawa amesema wao wamejikita katika kuwaidia watoto kwenye ulemavu na mahitaji ili waweze kupata elimu jumuishi. "Child Suport Tanzania na Shule ya Kimataifa ya Kifaransa uhusiano wetu umeanzia baada ya sisi kupata tuzo ya Haki za Binadamu kutoka Serikali ya Ufaransa na Serikali ya Ujeruman.

"Mahusiano yaliyopo ni muhimu sana katika kusaidia watoto Watanzania , pia nitoe shukrani kwa Shule ya Kifaransa kwa kuandaa tamasha hili kusaidia watoto wenye uhitaji .Tunahumia watoto 600 kwa Mkoa wa Mbeya lakini katika shule yetu tuna watoto 103 tunawaohudumia na kati yao watoto 73 ni watoto wenye ulemavu kwa hiyo harambee hii itakayofanyika Machi 26 itsaidia watoto katika sekta afya, usafiri na matengezo ya basi kwa ajili ya kubeba watoto pamoja na chakula.

Kwa upande wake Agusta Masaki ambaye ni Mbunifu wa Mavazi na Mmiliki wa Agusta Fashion Show.tz amesema kwenye shule hiyo ya Kifaransa wanafanya na watoto wenye ulemavu kwasababu anafuraha kufanya nao kazi ikiwa sambamba na kuwapata fursa ya kutambua vipaji vyao.

"Nawakaribisha Machi 26 mje muone vipaji vya watoto wenye ulemavu  na wale watoto wa kawaida tukishikiana na wabunifu wengine".


Guia Martinotti kutoka Noor Design (wakwanza kushoto) akizungumza kuhusu tamasha hilo na jinsi ambavyo wamejiandaa katika siku hiyo.Wengine kwenye picha hiyo  Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Kimataifa ya Kifaransa Rajab Katunda(katikatik) na wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Shule hyo Diana Neivasha.
Mrembo kutoka Vyuo Vikuu Otaiga Mwema(kushoto) akizungumza wakati wa kuzungumzia tamasha hilo litakalofanyika Machi 26 mwaka huu katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Kimataifa ya Kifaransa Rajab Katunda akiwa ameshika kipaza sauti .
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kimataifa ya Kifaransa (aliyesimama ) Caroline Martias akifafanua jambo wakati wa mkutano huo

Mrembo anayewakilisha Vyuo Vikuu Otaiga Mwema (kulia) akijadiliana jambo na viongozi wa Shule ya Kimataifa Kifaransa.
Noelah Msuya Shawa(kulia) ambaye kutoka Shirika la Child Support Tanzania akifafanua jambo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Kimataifa ya Kifaransa Diana Neivasha.

Viongozi wa Shule ya Kimataifa ya Kifaransa pamoja na baadhi wadau ambao watakuwa miongoni mwa watakaohudhuria tamasha hilo wakisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mwanamitindo Judith Ngussa (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Kimataifa ya Kifaransa Diana Neivasha(wa pili kulia) akielezea tukio la tamasha la 'Fashion Show' linalotarajia kufanyika Machi 26 mwaka huu.










Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini