CHANZO CHA MGONJWA MWENYE KISUKARI ALIYEKUWA BONGE KUKONDA SANA



Ushawahi Kuona Mgonjwa wa Kisukari Anavyokonda? Unajua ushauri anao ambiwa na watu? "Usibague Chakula ndio maana Unakonda" Ushauri huu Unakusindikiza kupoteza Maisha.

Kutokana na Uchakavu wa seli za mwili wa mgonjwa wa Kisukari seli hushindwa kutumia sukari kama awali kwa sababu ya Usugu na Uchakavu uliojengeka kwenye seli kwa miaka mingi (5-10), Insulin resistance.
.
Ubongo Ukisha baini seli za mgonjwa hazipokei sukari hutafuta njia mbadala ya kuzalisha sukari bila kujali wingi wa sukari kwenye damu. "Ubongo unahisi seli zinapungukiwa sukari kumbe uhalisia ni seli hazipokei sukari kwa sababu ya Hitilafu, Insulin resistance"
.
Mwili Huwa unatafuta njia mbadala ili kuhakikisha seli zinapata chakula na una endelea kuwa hai. Maamuzi ya Mwili ni Kuanza kutumia VYANZO MBADALA VYA KUZALISHA SUKARI. Na sukari Hii inayozalishwa huzalishwa kwa lengo Kwenda Kuzipa sukari seli ambazo Hazipokei sukari. Matokeo yake Ini litazalisha sukari na Hio sukari iliyozalishwa NAYO HAITATUMIKA kwa sababu SELI ZIMECHAKAA NA

 SELI ZINA USUGU KITALAMU INSULIN RESISTANCE.

.
Ndio maana mgonjwa wa Kisukari hata kama Ukifunga bila kula masaa zaidi ya 20 ukija Kupima sukari Unakuta iko Juu hata zaidi ya 20 mmol/L wakati uko kwenye mfungo na hujala Chochote. Inatoka wapi? Inatoka kwenye Ini.
.
Kadri asilimia ya seli ambazo hazitumii sukari (Insulin resistant cells) zinavyo ongezeka maana yake usugu wa kisukari Unashamiri Ndivyo na Ini Huongeza hasira ya Kutema Sukari.
.
Baada ya seli za mwili Kufanya mgomo wa kutumia sukari. Mwili hukimbilia KUCHOMA MAFUTA YA NDANI YALIYOHIFADHIWA. Kisayansi Mafuta ni Nishati mbadala Ya pili pale ambapo Sukari Imeisha au Haitumiki na Mwili. Kwa hio Utachoma mafuta Yote na baada ya mafuta Kuisha Mwili Hukimbilia nishati mbadala ya tatu Inaitwa PROTEIN ambapo sasa Mwili Utaanza KUCHOMA PROTINI YA VIUNGO VYA MWILI NA UTAANZA KUKONDA KWA SABABU MWILI UNAJITAFUNA.
.
Kasi ya Kuchoma Mafuta ya ndani Pale Ini linapokua linakunusuru usife kwa Kukosa Nishati ya Mwili inaweza kuwa Kubwa sana Kwa Mgonjwa endapo yupo kwenye hatua mbaya.
.
Je Kongosho Huwa Limekufa? Hapana! Kongosho huwa ni zima Lakini linaweza kupunguza uwezo wa kutema Insulin kwa sababu ya Kuchoshwa na Kazi kubwa ya Kukunusuri wewe usiitwe mgonjwa rasmi wa kisukari.
Kwa sababu seli za Mwili zimetengeneza Usugu wa Kugoma kupokea maelekezo ya Mratibu wa sukari mwilini (Insulin) basi Kongosho Huwa halitaki Kukubaliana na Hali hio iliyojengeka kwenye seli (Insulin resistance). Hivyo Kongosho Huongeza Juhudi Kutema Insulin Nyingi Nyingi Ili Kuondoa Kizuizi Hicho na Sukari Itumike na Itoke kwenye damu.
"Jamani mwili huwa unatupigania sana Tusiitwe wagonjwa wa Kisukari ila sisi kwa kutokujua tuna endeleza ulaji mbaya mpaka Kongosho Linakata tamaa kutupigania"
.
Kongosho Linapokua linapigana Kutema Insulin Nyingi kuondoa Kizuizi cha seli kugoma kutumia sukari husababisha Insulin Kuwa nyingi kwenye damu tunaita Compensatory Hyperinsulinaemia. Ni Dalili ya awali Ugonjwa Ukiwa unakuanza, Baada kongosho Kuchoka hupunguza uwezo wa kutema Insulin kwa kishindo kukupigani usiumwe kisukari hali hio Hulipata Kongosho huitwa Pacreatic Fatigue.
.
Kuchoka kwa Kongosho haina maana kongosho Limekufa ila Limetulia Kukupigania na Hii hali husababisha Insulin kupungua kwenye damu kwa kiwango kikubwa sana. Kongosho halijafa, Limechoka.
.
Kupungua kwa Kiwango cha Insulin kwenye damu husababisha Mgonjwa Kupungua kwa kasi ya ajabu na Hii inaweza kusababisha Kifo endapo Mgonjwa Asipopatiwa matibabu ya haraka KUZUIA MWILI KUJITAFUNA WENYEWE. Wakati mwili Unafanya hivyo Huzalisha Kampaundi ziitwazo Ketones Bodies ambazo zikiwa Nyingi zaidi ya mara 5 ya kiwango kinacho shauriwa kwenye damu Husababisha damu kuwa asidi na Kuathiri UBONGO NA VIUNGO VINGINE VYA MUHIMU NA KUSABABISHA KIFO.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini