Neno la leo toka kwa Dina Marios

 

Kijana Leo Nataka Nikwambie Mambo 2 muhimu yatakayo kusaidia katika afya yako ya akili.Mimi dada yenu nimefika hapa sio kwamba bado sikutani na mambo mengi yanayoweza kuniathiri hapana nakutana nayo.Ila nimejifunza kujisimamia na kusimamia misimamo yangu hata kama kuna watu hawatanielewa.

Kwanza Acha kuambatana na watu ambao kiukweli hawaelewi ndoto zako wala maono yako.Kuna mmoja juzi naongea nae ananiambia ana biashara ya kuuza pochi za mtumba baadhi ya marafiki na ndugu wanamcheka eti kwa biashara gani?mtumba?tena akipost status wana munch na kumfanya kichekesho.

Nikamwambia Ziba masikio acha kusikiliza distruction kadri unavyo sikiliza ndio wanakuletea negative energy mbaya utaanza kujikataa..FOCUS.Wewe ndio unajua why unafanya na wapi unaelekea ziba masikio,funga mkanda,fanya unachoamini hao wote wanasubiri ushindwe waseme kiko wapi?Songa mbele.Fanya yako uza karanga,Uza utumbo,uza matunda,zoa taka,zibua vyoo ni kazi yako ukikosa kipato watakupa?watakulisha?
.
Pili Kijana Huwezi kupendwa na kila mtu kuanzia ndugu,jamaa,marafiki.Iwe chuoni,Nyumbani,kazini,kwenye Biashara jifunze kuwa hutapendwa Na kukubalika na watu wote.
Tena kadri unavyokuwa utajua hata wale unaowatendea mema kila iitwapo Leo,wale wa karibu yako unaokula nao Na kucheka nao ndio wasio kupenda haswaa.Ubaya,Unafki huwa hautoki mbali ni kwa wale wa Karibu.
Roho za watu kama YUDA za unafki Na usaliti zipo zinaishi So Jifunze kuwa Acha watu kama walivyo.Pona kwenye Usaliti utakaokumbana nao.Jifunze na Zaidi Shukuru kwamba Umeweza kuwajua ili ujue wa kuishi nao (kwa Akili) Na wa kuwadelete kabisa.
Ishi Kwa Akili..Ishi Kwa Tahadhari..Ishi Kwa maarifa na taarifa...Relax usijichukulie serious sanaa mpaka unashindwa kufanya mambo kisa watu hawakupendi or wanabeza hustle zako..JIAMINI...And Enjoy.
Dina Marios

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini