N.I.T waibuka Mabingwa Bonanza la Diwani Mabibo | ZamotoHabari

 TIMU ya Mpira wa Miguu ya Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)imeibuka mabingwa katika Bonanza maalumu lililoandaliwa na Diwani wa Kata ya Mabibo baada ya kuifunga timu ya Azimio kwa magoli 3-0.

Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Loyola, mbali na mchezo wa mpira wa miguu ambao ulizishirikisha jumla ya timu 11, lilikuwa na michezo mingine ikiwemo mpira wa pete kwa wanawake, kukimbia, kuvuta kamba pamoja kufukuza kuku.

Kutokana na ushindi huo, timu hiyo ya N.I.T ilizawadiwa kikombe, seti moja ya jezi pamoja na mpira mmoja huku timu ya Azimio ambayo ndiyo imeshika nafasi ya pili ikizawadiwa seti moja ya jezi na mpira mmoja.

Akizungumza wakati wa bonanza hilo lililoudhuriwa pia na uongozi wa taasisi ya 'African Youth Empowerment' (AYE) inayojisghulisha na utafutaji wa vijana wenye vipaji vya mpira, Diwani wa Kata ya Mabibo Joseph Klerruu alisema lengo  lake ni kujenga umoja miongoni mwa wanajamii wa kata hiyo.

" Tumekutana hapa kwa nia moja ya kujenga ujamaa miongoni mwetu na kufahamiana, michezo ni undugu, urafiki hivyo naamini kupitia jumuiko hili la pamoja tunazidi kuukuza undugu wetu" alisema Klerruu

Alisema pamoja na hilo, kufanyika kwa bonanza hilo kumesaidia kujenga umoja na mshikamano miongoni wananchi wa kata hiyo ya Mabibo na majirani zao huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kujiandaa na Sensa inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa wananchi kujitokeza na kushiriki katika sensa hiyo ili kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada anazozifanya kuliletea maendeleo Taifa hili.





 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini