RAIS SAMIA ATWAA TUZO YA HESHIMA TMA | ZamotoHabari

Khadija Seif na Humphrey Shao, Michuzi Tv

Kutoka katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ambapo leo Aprili 2, 2021 kunafanyika hafla ya utoaji tuzo za muziki zilizoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia BASATA ambapo tukio limeanza kwa kutoa tuzo za heshima na tuzo maalum iliyotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini mchango wake mkubwa katika sekta ya sanaa nchini.

 Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Matiko Mniko akizungumza na wadau wa Muziki na wageni waalikwa katika kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere katika hafla ya utoaji Tuzo ambapo tayari amegawa Tuzo za  Heshima 4.

Mniko amemtaja Msanii wa Bongofleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond platinum Kwa kutambua Mchango wake katika Muziki wa Bongofleva na kuleta Mapinduzi makubwa na kupelekea Muziki wa Bongofleva Kimataifa na kushirikiana na wasanii mbalimbali wa Kimataifa.

Aidha, Miongoni mwa waliopokea Tuzo za heshima ni pamoja na Mkuu wa Majeshi CDF Jenerali Venance salvatory Mabeyo Kwa Mchango mkubwa uliofanyika katika Vita Vya Uganda na nyimbo nyingi kutungwa kipindi hiko ikiwa ni sehemu ya kuendelea kukuza Muziki nchini.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Matiko Mniko akizungumza na wadau wa Muziki na wageni waalikwa katika kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere katika hafla ya utoaji Tuzo ambapo tayari amegawa Tuzo za  Heshima 4.
Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo Mohamed Mchengerwa akizungumza na Wadau wa Muziki
Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezi Mohamed Mchengerwa akiwa ameshikilia tuzo ya Heshima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassan ambayo amepewa na Chama cha Muziki wa Dansi nchini
Katibu Mtendaji wa Chama cha Muziki wa Dansi Agape Msumari akikabidhi Tuzo ya Heshima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  kwa Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezi Mohamed Mchengerwa








Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini