YANGA SC YAENDELEZA UBABE MBELE YA AZAM FC,YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI | ZamotoHabari


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WANANCHI!!! Young Africans SC wameendeleza ubabe mbele ya Azam FC kwa kuchukua alama sita msimu huu wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, baada ya kupata ushindi wa bao 2-1 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Wakiwa Viongozi wa Ligi hadi sasa, Yanga SC walipata ushindi huo wa bao 2-1, kwa mabao ya Wachezaji wake Djuma Shabani kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 17 na bao la ushindi likifungwa na Mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 78 huku bao la Azam FC likifungwa na Rodgers Kola dakika za mwanzo za mchezo huo.

Yanga SC sasa wamejichimbia kileleni, wamejikusanyia alama 51 na michezo 19 huku Simba SC wakifuatia wakiwa na alama 37 michezo 17 na Azam FC wenye alama 28 na michezo 18 pekee.

Mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi Kuu, Yanga SC walishinda bao 2-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.




 



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini