Na Khadija Seif, Michuzi TV
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mfaume Mfaume amewahidi watanzania kufanya vyema katika pambano la ''The Return of Nakoz King" dhidi ya Abdumonem Said kutoka nchi ya Misri pambano litakalofanyika Juni 10 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo la kuwania mkanda wa Ubingwa wa WBF lenye raundi 10 uzani wa kilo 69 litalopiganiwa Kwa ajili ya kupambania mkanda huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mfaume amesema atafanya vizuri katika pambano hilo kwa ajili ya kushinda mkanda huo.
"Nimejiandaa vizuri sina wasiwasi maana nimekaa nje ya ulingo zaidi ya mwaka moja na miezi sita, nitaonyesha mchezo mzuri na kukutana na mtu wa hatari, " alisema Mfaume.
Bondia huyo anatarajia kuanza Kambi hivi karibuni Kwa ajili kujiandaa kikamilifu chini ya Kocha wake, Rama Jah.
"Nawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika pambano hilo, pia nawahidi kufanya vema katika huu mchezo ili kuwakikishia watanzania nitafanya vyema, " alisema Mfaume.
Kocha wa bondia huyo, Raha Jah atahakikisha anamundaa vyema bondia wake ili kuonyesha mchezo nzuri siku hiyo.
Pia ameeleza kuwa wataingia kambini ili kujinoa kikamlifu na kumpa silaha kali bondia wake kwa lengo la kubakisha mkanda huo nyumbani.
Muaandaji wa pambano hilo, Siah Mosha amesema mapambano ya utangulizi yatakuwa manne kwa ajili ya kusindikiza pambano hilo.
Amesema pambano hilo ni kubwa kutokana na uzito wa mabondia ambao wanacheza na historia nzuri.
"Nawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika pambano hilo, kwani viingilio vya tiketo vitatangazwa hivi karibuni ili wadau na watanzania wajitokeze siku huiyo, " alisema.
Muandaji huyo alitaja mapambano ya utangulizi Oscar Oscar atazichapa na Hassan Milanzi kutoka Zimbambwe, Juma Choki akichuana na Issa Nampepeche kwa ajili ya kuwania mikanda ya PST na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC).
Wengine ni Stumai Muki akipepechana na Chimwemwe Banda na Hasimi Maya atapigana na Mudochee Katembo kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC).
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments