MISS TANZANIA HAPATOSHI MLIMANI CITY,KUFANYIKA MEI 20 MWAKA HUU | ZamotoHabari



Na.Khadija Seif Michuzi TV

KILELE cha Kumsaka Mrembo wa kitaifa (Miss Tanzania) kinatarajia kutimua kivumbi cheke rasmi mei 20 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Matiko Mniko amewaasa warembo kutumia jukwaa la urembo kama njia rahisi ya kuonesha vipaji vyao vya ziada kwani milango mingi hufunguka huku akisisitiza suala la nidhamu.

"katika Shindano ambalo Kwa mwaka watu walikua wanasubiria Kwa hamu sana ukiachana na ushabiki wa simba na yanga basi inafatia Miss Tanzania na Kwa bahati nzuri naona mwaka huu vyuma vipo "

Hata hivyo Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu ametoa wito Kwa warembo kutumia vipaji vyao kama fursa ya kujitangaza.

"Wito wangu Kwa wadau ni kwamba Mashindano haya ni Kwa ajili ya kuikuza Sekta ya urembo lakini pia kuunga Mkono juu Serikali, tumekuwa mashuhuda kupitia Mashindano ya urembo nchi inapata nafasi ya kutangazika .

Kwa upande wa Mkurugenzi wa chaneli ya st bongo Isaya Kandonga amesema wameshiriki vikao mbalimbali vikishirikisha waandaji wa Shindano hilo "The look " takribani vikao vinne vyenye lengo la kuona Kwa jinsi gani shughuli hiyo inakua ya kitofauti zaidi kuliko misimu iliyopita.

" Msimu huu wa Shindano hilo litakua la kitofauti kuanzia kimaudhui kwani washiriki hao 20 wataanza kuonyeshwa shughuli zao zote wakiwa kambini Hadi kufikia siku ya fainali yenyewe hivyo watazamaji wataona warembo hao Kwa namna wanavyoishi wakiwa kambini ,tabia,na hata jinsi warembo hao wakipika vyakula mbalimbali."

Kandonga ameeleza kuwa Kwa wadhamini walioshiriki na watakaopendezewa kushiriki katika Shindano hilo Kwa mwaka huu watatendewa Haki Ili Kwa mwaka mwengine wadhamini wengine waweze kujitokeza zaidi.

Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes ameongeza kuwa zawadi ya atakaeibuka Mshindi ni zaidi ya Million 20 na kuomba wadhamini kujitokeza na kujinasibu kuwa jukwaa Litasheheni Utamaduni wa kinyumbani zaidi ambapo litafungwa na wakali wa kazi za mapambo hugodomingo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Azma Mashango amesema Shindano la Miss Tanzania litafanyika mei 20 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam.

Aidha,ametoa ufafanuzi kuhusiana na Mrembo alieteuliwa kushiriki Miss world Juliana Rugumisa kuwa anaendelea na dili alilopata nchini italia mara baada ya kutofanikiwa kushinda Miss world .

Warembo 20 wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Shindano la Miss Tanzania akiwemo Miss Tanzania 2021 Rose Manfere,Warembo wa shindano hilo   tayari wameingia kambini kujinoa zaidi huku wakielekea kwenye fainali inayotarajiwa kufanyika Mei 20 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini