MREMBO MISS UTALII JUDITH NGUSA KUIWAKILISHA TANZANIA FAINALI ZA DUNIA SHINDANO LA MISS UNITED NATION 2022 | ZamotoHabari

UJIO mpya wa shindano la Miss Utalii Tanzania, umefungua milango ya Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia ushiriki wa washindi wa shindano hilo katika fainali za dunia za mashindano mbalimbali ya urembo wa kitalii na kitamaduni.

Ikumbukwe waandaaji  wa shindano hili, wamefanya kazi kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia shindano hilo la Miss Utalii Tanzania kwa washindi wake wa kitaifa na wengineo wa ngazi mbalimbali kushiriki na kushinda mataji ya dunia katika fainali za dunia za mashindano mbalimbali.

Juhudi hizo ambazo zimekuwa na manufaa makubwa yamesababisha Tanzania kupewa heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za dunia za Miss Utalii Dunia 2006.

Kwa mujibu wa wadau wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania wanaeleza kwamba baada ya kusitishwa kwa muda mwaka 2013/2014, na kuanza upya mwaka 2020/2021 baada ya kuboresha mfumo wa shindano na uongozi, tayari  matunda yake yameanza kuonekana kwa kuanza kupeleka washindi wake wa mwaka 2021/2022 katika mashindano mbalimbali ya dunia ya urembo wa kitalii na kitamaduni.

Hivyo Mshindi wa pili wa Miss Utalii Tanzania 2021/2022, Judith Peter Ngusa tayari ameondoka nchini kwa Shirika la Ndege Ethiopia Airline kwenda nchini India kwa ajili ya kushiriki shindano kubwa la fainali za dunia za Miss United Nation 2022 zitakazofanyika Mei 8 mwaka huu katika Jiji la New Delh nchini humo.

Mwakilishi huyo wa Tanzania amekwenda kwenye shindano hilo kwa udhimini wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) na kwamba akiwa huko ataungana na watembo wengine 70 ambao wanashiriki shindano hilo kwa kuziwakilisha nchi zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa mashindano hayo akiwemo Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano Georgina Saulo kwa niaba ya Menejimenti yake ameishukuru TFS kwa kufanikisha ushiriki wa warembo wa Miss Utalii Tanzania katika fainali hizo za dunia na kuahidi kuwa kutokana na udhamini huo wawakilishi hao watatumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii Ikolojia na aina nyingine ya utalii ulioko chini ya TFS.

“Kwa udhamini huu ambao tumeupata akiwa huko mwakilishi wetu atatangaza vivutio vya utalii na uwekezaji wa kitalii vya Tanzania, lakini ajenda yake kuu ikiwa ni kutangaza vivutio vya utalii wa kiikolojia (TFS – Tanzania Eco Tourism tourist destinations) vya Tanzania kupitia ushiriki wake katika fainali hizo za dunia nchini India,”amesema.

Kwa upande wake Rais wa Miss Tourism Tanzania Beauty Pageant,Erasto Gideon kwa niaba ya bodi , amatoa shukurani na pongezi kwa uongozi na wafanyakazi wote wa TFS  kwa kutambua na kuthamini mchango wa Urembo wa kitalii na kitamaduni katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii na uhifadhi, hususani Utalii wa Kiikolojia, Maeneo ya Urithi wa Taifa na Kitamaduni.

Aidha amesisitiza warembo wa Miss Utalii Tanzania mwaka huu wamealikwa na kupewa heshima ya kushiriki katika zaidi ya mashindano kumi ya dunia na mengineyo ya kimataifa, katika nchi mbalimbali duniani barani Ulaya,Amerika,Asia na Afrika.

“Hii ni fursa  kwa Tanzania na TFS kujitangaza kimataifa kwani kilashindano linashirikisha wastani wa nchi 100. Kitaifa tumeandaa program maalum ya promosheni ya utalii wa kiikolojia, mali kale, hifadhi za misitu za majini na nchi kavu itakayo julikana kama “Tanzania Eco Tourism and Conservation Great Safari Tour”.

“Hatua  hii ni utekelezaji na uungaji mkono kwa vitendo juhudi za serikali na mamlka zake za utalii na uhifadhi ikiwemo TFS katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii na uhifadhi, kama ilivyo idhihirishwa na kupambanuliwa katika filamu ya Tanzania Royol Tuor iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan , Ilani ya CCM ya 2020-2025 na hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Pindi  Chana alipo tembelea makao makuu ya TAWA.”

Kwa mujibu wa wadau hao ni kwamba kwa maandalizi waliyoyafanya wanaamini  Judith Peter Ngusa sio atawakilisha vyema Tanzania tu, bali atadumisha na kuendeleza rekodi ya Miss Utalii Tanzania ya kushinda mataji katika mashindano yote ya dunia na kimataifa waliyoshiriki  na kuwakilisha Tanzania.

Hivyo wamewaomba  watanzania wote kumuombea  ashinde taji la  Fainali ya Miss United Nations 2022, zinafanyika New Delh India tarehe 8-5-2022.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini