MTANZANIA KUWAKILISHA MCHEZO WA POOL 'PAUL POOL GRAND OPEN' NCHINI UGANDA | ZamotoHabari


MCHEZAJI wa Pooltable anayeshikilia kiwango cha namba moja Tanzania, Abdallah Hussein(Dullah) leo mapema ameondoka kuelekea Uganda kwenye Mashindano ya wazi "PAU Pool Grand Open" yaliyoandaliwa na Chama cha Pool nchini Uganda(PAU).

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii May 28 - 29, 2020 katika Ukumbi wa SEETA Kampala Uganda kwa kushilikisha Wachezaji nguli(Maarufu) Afrika ambao tayari wameshathibitisha kushiriki.

Wachezaji waliothibitisha kushiriki ni kutoka, Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Tanzania na wenyeji Uganda.

Abdallah Hussein (Dullah) ametamba kwenda kufanya vizuri kwenye mashindano hayo baada kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki hivi karibuni yaliyofanyika Nchini Kenya nakupata uzoefu wa kutosha.

Alisema Dullah, 'Nina ndoto za mbali sana za kuitangaza Nchi yangu ya Tanzania kupitia mchezo wangu wa Pool, naomba sana Wafadhili wangu, ndugu zangu, marafiki zangu na Watanzania kwa ujumla mniombee' alimaza Dullah huku akiingia kwenye Bus likielekea Kampala Uganda.




 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini