MWILI KUWA KWENYE MSONGO WA SUMU

Unapokuwa unafanya kazi katika Mazingira ya Kukaanga vyakula kwa kutumia mafuta ya mbegu unakuwa hatarini sana Kuugua Matatizo ya Kifua (Asthma) Pumu ya ngozi na Magonjwa mengine ya Kuvimba kwa mwili ndani yani Inflammatory Autoimmune Disorders kama Osteoarthritis,Rheumatoid arthritis (Baridi yabisi),Autoimmune Thyroid disorders (Graves' disease na Hashimoto's thyroiditis) nk


Free Radicals Ni Molekyuli za Oksijeni ambazo huwa zipo huru na zina tabia za Kuleta majeraha/Kuumiza viungo vya mwili.
.
Kumbuka Miili yetu imetengenezewa uwezo wa Kusafisha mabaki haya ya Oksijeni Free Radicals Automatic kwa kutumia Viondoa sumu Ant Oxidants Lakini Inapotokea Vile viondoa sumu Vikatumika vyote mwili wako utazidiwa Mabaki haya ya Oksijeni Free Radicals na Mwili wako utasemekana uko kwenye msongo wa sumu OXIDATIVE STRESS.
.
Kumbe Mwili Una mfumo wa Kusafisha damu kwa kutumia Viondoa sumu. Ila pale vyanzo au utengenezaji wa Free radicals ukawa wa kishindo mwili huingizwa kwenye Msongo wa Sumu Free Radicals.
.
MAMBO HATARISHI: NIMEELEZA KWA KINA KWENYE KITABU CHA SAYANSI YA MAPISHI.
1. Matumizi ya Vyakula Vilivyo Kaangwa kwenye Mafuta Dhaifu kwenye Moto Mkali.Yani Polyunsaturated Fat acids (PUFA).
Alizeti Pamba soya Mahindi nk
2. Kufanya Kazi Za Kukaanga vyakula Kwenye Mafuta yasiyo na uwezo mkubwa kuhimili moto. Kukaanga Chips Mandazi Kupika chapati Kukaanga kuku nk
3. Matumizi ya Vyakula vyenye Mafuta ya Mgando ya Mbegu za Mimea. Margarine.
4. Mgonjwa wa kisukari Endapo asipodhibiti sukari Mwili huzalisha Free Radicals nyingi na kuingia kwenye msongo wa sumu.
.
Mwili unapokuwa kwenye Oxidative Stress mashambulizi Yanaweza kuelekezwa kwenye:-
1. Mishipa ya damu Ukapata Presha kali Kipanda uso na Hata Kiharusi
2. Njia za Hewa:Kifua kinakuwa kinabana dalili zote za Pumu.
3. Ngozi :Kupata Mzio mwili mzima au Chunusi nyingi zenye usaha Usoni
4. Joints Hukauka Ute, Kusagika na Kupata mashambulizi nk
.
Watu wengi sana Wako kwenye Oxidative stress na Wanateseka na Magonjwa yasiyo Simulika. Unakuta una Dawa Mfuko mzima kwa sababu Unatibu DALILI ZA MWILI KUWA KWENYE OXIDATIVE STRESS. Je ni Lini Utaanza Kushughulikia MZIZI WA MARADHI.

Na

Dr. Boaz Mkumbo MD


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini