Nimeileta kama ilivyo!

Nina mtoto wa miaka miwili, Baba wa mtoto tulishaachana naye, ana mwanamke wake na nahisi mwaka huu wanafunga ndoa. Sababu ya kuja ni hivi, amekua akija kwangu kumuona mtoto, anataka kukaa ndani kucheza na mtoto.
Ingawa anahudumia lakini mimi sioni sawa kwani kila mtu anaona kama bado niko naye, nikimuambia tuwe tunaonana nnje ya nyumbani anakataa na kunitishia kuwa hatahudumia mtoto, naomba unisaidie sijui nifanye nini?
JIBU LANGU; Tafuta kazi uwe unajiweza kikipato kiasi kwamba hata asipokuhudumia mwanao hafi njaa. Baada ya hapo muambie kuwa hwezi kuonana naye kwako, ishi maisha yako.
Kama atagoma kuhudumia nenda ustawi wa jamii, haisaidii sana ila muhimu ajue kuwa huwezi kusimamisha maisha yako kwajaili yake.
Ukiendeleza hivyo kumruhusu Baba wa mtoto kuja kwako ni ngumu sana kupata mwanaume mwingine wa kukuoa, yeye maisha yake yataendelea ila yako yamesimama.
Mwisho utajikuta una mimba yake nyingine wakati yeye ana famiia yake, baadaye anakuacha kabisa unaishia kulia tu!
NB: Soma “HAKUNA KUACHWA ACHWA”

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini