WASHINDI WA UNI TALENT WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO | ZamotoHabari


   Na.Khadija Seif,Michuzi TV

BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) limewataka wanafunzi vyuoni kutumia fursa zinazopatikana  kwenye Mashindano ya kusaka vipaji nje na ndani ya nchi Ili kutimiza ndoto zao .

Akizungumza hayo wakati wa kukabidhi zawadi Kwa washindi wa Shindano la Uni talent ,Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka  (BASATA) Agustino Makame amesema wanafunzi vyuoni wanatakiwa kuzikimbilia fursa kikamilifu hususani Mashindano ya kusaka vipaji Ili kuendeleza vipaji vyao pamoja na kukuza tasnia ya burudani nchini.

"uwepo wa Mashindano ya kusaka vipaji ikiwemo ya "Uni talent" ni ishara tosha kuwa wanafunzi vyuoni Wana uwanda mpana wa kuonyesha vipaji vyao na kuendeleza vipaji hivyo kutokana na wengi wao kuendelea kupeperusha vyema bendera ya burudani hivyo ni muhimu kwao kuzikimbilia fursa hizo."

Hata hivyo Afisa huyo ametoa wito Kwa wadau na Makampuni kuunga Mkono vipaji vyuoni na BASATA kushirikiana na Kampuni iliyoandaa Shindano hilo ya Maroon entertainment kuwa bega Kwa bega kuhakikisha Msimu ujao unakua wa kitofauti zaidi.

Mkurugenzi wa Kampuni iliyoandaa Shindano la "Uni talent" Chrispine Kiondosha  amesema  hatimae wanahitimisha Msimu wa 3 na kuhakikisha washindi wanakabidhiwa zawadi zao.

Pia ameeleza kuwa Shindano hilo litakua endelevu ili kuhakikisha wanaendeleza vipaji Kwa wanafunzi vyuoni na msimu wa 4 unakua msimu mzuri.

Aidha katika makabidhiano hayo mshindi wa kwanza ni kutoka Chuo cha Sanaa Cha Bagamoyo (TaSUBa),  "African cousins" wakiondoka hundi ya shilingi milioni 10 pamoja na nafasi ya kusoma nje ya nchi, Mshindi wa pili "Afro dreams" wamekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 5 na nafasi ya tatu ikishililiwa na  Osmond Soka akikabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 1.
 

Mkurugenzi wa Maroon entertainment Chrispine Kiondosha, ambae pia ndio Mratibu wa Shindano la "Uni talent" akizungumza na waandishi Wahabari Jijini Dar es salaam  mara baada ya kukabidhi zawadi Kwa washindi watatu katika Shindano hilo.

 Mshindi wa tatu Osmond Soka katika akisikiliza kwa makini namna mchakato ulivofanyika Hadi kupatikana Kwa washindi wa Shindano la "Uni talent"

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini