UBALOZI wa Ufaransa nchini kwa kushirikiana na WePresent Tanzania wameandaa tamasha Hip Hop asili kwa msimu wa pili litakalofanyika kwa siku tatu za Juni 23 hadi 25 kuanzia saa tano asubuhi hadi saa sita usiku katika ukumbi wa Alliance Francaise jjini Dar es Salaam kwa kiingilio cha shilingi 10,000 kwa siku na shilingi 20,000 kwa siku tatu za tamasha hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati kuzindua msimu wa pili wa tamasha hilo Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema kuwa, tamasha hilo litawaweka vijana pamoja na kuwakilisha mawazo yao kupitia sanaa pamoja na kujitangaza.
''Tanzania, nchi za Afrika Mashariki, Marekani na Ufaransa watashiriki tamasha hili na kuleta thamani juu ya sanaa ambayo hudhaniwa ni kwa ajili ya kundi la wanaume pekee au kwa ajili ya kundi fulani, tutashuhuda sanaa za deejaying, MC's tutegemee burudani kwa siku tatu za tamasha hili.'' Amesema Balozi Nabil.
Aidha amesema kuwa tamasha hilo limeungwa mkono na ubalozi wa Ufaransa Tanzania, Alliance Francaise Dar es Salaam pamoja na ubalozi wa Marekani Tanzania na ni mwendelezo wa tamasha lililofanywa na wana Hip Hop 30 wa Afika na Ufaransa Oktoba mwaka jana katika mkutano wa New Africa-Fance Summit (NSAF,) ambao ulichochea kuandaliwa kwa mkakati wa ushiriki wa Hip Hop kwa bara la Afrika kwa mwaka 2022/2024.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha utamaduni cha Alliance Francaise Frola Valleur amesema kuwa, tamasha hilo limelenga kujenga ushirikiano pamoja na kutangaza sanaa na tamaduni za Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla ulimwenguni.
Amesema tamasha hilo la siku tatu limeandaliwa mahususi katika kusherekea utamaduni wa Hip Hop Afrika Mashariki na litaambatana na sanaa nyingine nyingi ikiwemo breakdancng, emceeing, graffiti, deejaying, beeat boxing pamoja na boarding.
''Siku ya tarehe 24 Juni kutakuwa na shindano la break dance la Afika Mashariki na kupata bingwa wa Tanzania ambaye atawakilisha kwenye 'Battle of the Year 2022 ' nchini Japan, siku ya tarehe 25 tamasha litapambwa na wasanii Octopizo kutoka Kenya, Tina Mweni wa Kenya/ Denmark, Rise up Band ya Tanzania/ Ufaransa, Jay Moe wa Tanzania, The Mc 255 wa Tanzania, Mic Crenshaw wa Marekani, Lord Eyes wa Tanzania pamoja na wengine wengi watapamba tamasha hili.'' Amesema.
Aidha amesema, warsha hiyo ya siku tatu litabeba maudhui mbalimbali ikiwemo historia ya Hip Hop Tanzania, sanaa ya emcee, breakdance, beat box kupitia wawezeshaji Bboy Lilou kutoka Ufaransa ambaye pia ni bingwa wa dunia wa breakdance pamoja na Deejay PH wa Ufaransa, Mejah Mbuya wa Tanzana pamoja na Mama C wa Tanzania/ Marekani.
Amesema kituo hicho cha utamaduni kilianzishwa mwaka 1961 nchini kwa malengo ya kufundisha lugha ya Kifaransa ambapo mwamko wa watanzania ni mkubwa pamoja na kueneza utamaduni wa Tanzania ulimwenguni.
''Tanzania ina mwamko mkubwa wa kujifunza Kifaransa hadi sasa tuna wanafunzi wapatao 450 na katika kueneza utamaduni wa Tanzania katika msimu huu wa tamasha la pili na HipHop asili wasanii kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Kongo, Ghana, Ufaransa na Marekani wataungana na wanamuziki 36 waliochaguliwa kupitia mashindano ya Hip Hop asili kutoka mikoa sita ya Tanzania ikiwemo Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar.'' Amesema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Alliance Francaise Mkuki Byoga ameeleza kuwa kwa miaka 20 sasa sanaa imekuwa kwa kasi ikiwemo muziki wa Bongo Flavour ambao umekua kupitia sanaa ya Hip Hop na kuchangia katika pato la taifa na kupitia jukwaa hilo itaiweka Hip Hop hai zaidi na kwa nchi za Afrika ambazo pia zinashiriki katika tamasha hilo na duniani kwa ujumla.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (katikati,) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa tamasha la Hip Hop asili 2022 na kueleza kuwa tamasha hilo litawaweka vijana pamoja na kuwakilisha mawazo yao kupitia sanaa pamoja na kujitangaza. Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kituo cha utamaduni cha Alliance Francaise Frola Valleur (katikati,) akizungumza wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa tamasha hilo limelenga kujenga ushirikiano pamoja na kutangaza sanaa na tamaduni za Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla ulimwenguni.
Muongozaji wa tamasha hilo Mathieu Bruno (kushoto,) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa wamejipanga na wanatumaini kupata matokeo chanya ya tamasha hilo kwa mwaka 2022.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Alliance Francaise Mkuki Byoga (katikati,) akizungumza wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa kwa miaka 20 sasa sanaa imekua kwa kasi ikiwemo muziki wa Bongo Flavour ambayo imekua kupitia kupitia sanaa ya Hip Hop na kuchangia katika pato la taifa kwa kiasi kikubwa. Leo jijini Dar es Salaam.
Matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments