BASATA YAKABIDHI VYETI KWA WANDAAJI NA WADHAMINI WA MISS TANZANIA 2022 | ZamotoHabari



Na.Khadija Seif, Michuzi Tv


BARAZA la sanaa la Taifa (BASATA) lime wapongeza waandaaji na wadhamini wa shindano la Miss Tanzania 2022 kwa kukamilisha mchakato wa mchuano huo kwa viwango vya juu.

Ambapo Shindano hilo lilifanyika Mei 20 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam, na Mrembo alieiwakilisha kanda ya kusini Halima Ahmad Kopwe, aliibuka mshindi na kukabidhiwa gari yenye thamani ya milioni 40 na fedha milion 10 kwa ajili ya maandalizi ya shindano la dunia.

Akizungumaza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam, kaimu Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa(BASATA) Matiko Mniko amesema wamefurahishwa na uendeshaji wa shindano hilo kuanzia maandalizi Hadi kukabidhiwa zawadi Kwa washindi.

"Kwa niaba ya Serikali niwapongeze wandaaji wa shindano hili The Look Company Limited, pamoja na wadhamini Startimes, kwa kuandaa shindano lenye hadhi na viwango vya juu na kutoa zawadi zenye thamani ya kuheshimisha tasnia ya urembo hapa nchini sisi kama Baraza la Sanaa tuna watunuku vyeti vya pongezi na barua."

Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Azama Mashango, amesema wanamefarijika kwa kuwa kuona walezi watasnia (BASATA ) wametambua kazi yao na kuomba waendelee kuwashika mkono ili kukuza tasnia ya urembo.

Kwa upande wa Mdhamini Mkuu wa Shindano hilo kutoka Kampuni ya startimes Meneja Masoko David Malisa amesema tayari wameanza kujiandaa kwa msimu mpya wa shindano hilo kwa sababu wanataka kufanya vizuri zaidi.

"Tunashukuru kwa pongezi za Basata tumezipokea na tuna ahidi kuboresha zaidi shindano hilo tumejipanga kwa msimu ujao tutaanzia ngazi ya mkoa, kanda mpaka Taifa ili kuboresha Shindano hili zaidi na inavotakikana."

 

picha ya pamoja kati ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Msaidizi wake Bona Masenge , Mdhamini Mkuu wa Shindano hilo Startimes akiwakilishwa na David Malisa, Mdhamini quantum infinity Yusuf Kamote pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Azam Mashango pamoja na Mshindi wa Halima Kopwe na warembo wengine Angel Mtatiro na Otaigo Mwema
Meneja Masoko wa Kampuni ya startimes David Malissa akizungumza machache mara baada ya kutambulika rasmi udhamini wake na Mchango wake wa viwango vya juu kufanikisha Shindano la Miss Tanzania mwaka 2022 linafanyika kitofauti zaidi
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Azama Mashango akitoa neno la shukrani Kwa baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kwa kutambua mchango wa Sekta ya urembo nchini na kutoa ushirikiano Hadi kufanyika kwa Shindano la Miss Tanzania mwaka 2022
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini