Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
MABONDIA wataofanya vizuri katika pambano la 'Usiku wa Kisasi' ambalo litafanyika Juni 25 mwaka huu watapata nafasi ya kucheza katika pambano la marudiano kati ya Bondia kutoka Kongo Tshimanga Katompa dhidi ya Selemani Kidunda kutoka Tanzania litakalofanyika Julai 30 mwaka huu Songea mkoani Ruvuma.
Akizungumza mara baada ya kumalizika Kwa zoezi la mwisho la kupima uzito kwa Mabondia watakaopanda ulingoni pambano la "Usiku wa kisasi" Muandaaji wa pambano hilo, Meja Selemani Semunyu amesema Miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la Selemani Kidunda dhidi ya Tshimanga Katompa na Ally Ngwando atapanda ulingoni dhidi ya Yusuph Ally raia wa Malawi.
"Mabondia wataofanya vizuri watapata nafasi kucheza katika pambano la Selemani Kidunda dhidi ya Tshimanga Katompa, pambano la kwanza ni Ally Ngwando atacheza na Yusuph Ally hii baada ha kuonyesha nidhamu na kufika Kwa wakati katika zoezi hili la kupima uzito na Hamidu kwata kuingia mitini."
Muandaji huyo wa pambano amesema mabondia zaidi ya 32 wamepima uzito kuelekea katika pambano hilo na kuendeleaa kuonyesha tambo zao.
"Nawaomba wadau na mashabiki wa ndondi kujitokeza kwa wingi katika pambano hili ili kuja kushuhudia mtanange mkali kutoka kwa mabondia chipukizi wa mitaani ambao hawakupewa nafasi kuonyesha vipaji vyao.
Upande wa bondia, Ally Ngwando amesema amejipanga kikamilifu kuonyesha mchezo mzuri katika pambano hilo dhidi ya mpinzani wake Hamidu Kwata.
Mabondia hao watacheza pambano la kuwania mkanda wa Ubingwa wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) lenye raundi 10 uzani wa kilo 56.
Aidha Ngwando ameongeza kuwa awamu hii amejipanga vizuri Ili kuondoa utata na kuweka historia ndani ya Ukumbi wa Ndani wa Taifa.
Bondia Ally Ngwando akiweka tambo za mwisho kuelekea pambano la "usiku wa kisasi" mapema Juni 25 katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo Ngwando atazichapa na Hamidu kwata
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments