MANÉ AONDOKA LIVERPOOL NA REKODI YA AINA YAKE | ZamotoHabari

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal, Sadio ManĂ© (30) rasmi amekabilisha uhamisho katika Klabu ya Beyern Munich ya Ujerumani kwa mkataba wa miaka mitatu uliotajwa kuwa na thamani ya £35M akitokea Klabu ya Liverpool ya Uingereza, ambapo alisajiliwa msimu wa mwaka 2016 kutoka timu ya Southampton ya nchini Uingereza.

ManĂ© akiwa Liverpool alicheza michezo 269 ndani ya misimu 6 na alifanikiwa kufunga mabao 120 katika mshindano yote, sanjari na Pasi za mabao (Assists) 38 pekee. 

Akiwa na misimu 6 ndani ya Liverpool, Mané amefanikiwa kutwaa mataji ya Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (EPL), Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CL), Kombe la Dunia ngazi ya Vilabu (FIFA Club World Cup), UEFA Super Cup, Emirates FA Cup na Carabao Cup.

Kupitia tovuti rasmi ya Liverpool, Kocha Mkuu wa timu hiyo, JĂ¼rgen Klopp amenukuliwa akisema Mshambuliaji huyo raia wa Senegal ni ‘Mashine’ kwa kile alichokifanya kwenye Klabu ya Liverpool muda wote alipokuwa hapo.

Tangu aliposajiliwa na Liverpool mwaka 2016 alikuwa Mchezaji tegemezi katika Kikosi cha kwanza (First Squad) ambapo aliisaidia timu hiyo kufika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Soka nchini Uingereza msimu wa 2016-2017 akiwa mmoja wa Wafungaji bora na Nyota Philippe Coutinho na kuifanya Liverpool kurejea kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kiwango cha Mshambuliaji huyo kiliendelea kukua mwaka hadi mwaka, akiwa kinara wa upachikaji mabao Liverpool. Msimu wa mwaka 2017-2018, Mané alifunga mabao 20 katika mashindano yote ambayo Liverpool ilicheza, mabao 10 katika Ligi Mabingwa Ulaya ambapo Majogoo hao wa London walifika Fainali ya Michuano hiyo kwa kucheza na Real Madrid mjini Kyiv nchini Ukraine, ambapo Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Msimu uliofuata wa mashindano hayo ya Ulaya, Liverpool walifanikiwa kutwaa taji hilo mbele ya Tottenham Hospur baada ya ushindi wa mabao 2-0 kwenye dimba la Wanda Metropolitano mjini Madrid nchini Hispania. Katika msimu huo Mané licha ya kuisadia Liverpool kutwaa taji hilo, alifikisha mabao 22 katika Ligi Kuu nchini Uingereza na kushida Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot) akiwashinda Mohamed Salah na Pierre-Emerick Aubameyang.

Akiwa Mchezaji Bora wa msimu barani Afrika mwaka 2019 aliisaidia tena Liverpool kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2019-2020 akiwa na mabao 22 na ‘assists’ 12 kwenye mashindano yote ambapo pia walishinda mataji ya Kombe la Dunia ngazi ya Klabu (FIFA Club World Cup) na UEFA Super Cup.

Msimu wa 2020-2021, licha ya ukame kwenye Klabu ya Liverpool, Sadio Mané aliisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa EPL, akifunga mabao mawili katika mchezo wa mwisho wa mashindano, baada ya Mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani kutokana na janga la COVID-19.

Katika mafanikio hayo, Mané akiwa Liverpool, msimu wa 2021-2022 aliisaidia timu yake ya Taifa ya Senegal kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Cameroon.






Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini