HAJI MANARA MATATANI KWA UKIUKWAJI WA MAADILI | ZamotoHabari


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Haji Manara yupo matatani akituhumiwa kwa vitendo vya ukiukaji wa maadili wakati wa mchezo wa Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Coastal Union FC ya Tanga, kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Katika mchezo huo, Haji Manara anadaiwa kulumbana na kurushiana maneno na Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Wallace Karia, kitendo kilichonukuliwa ni ukiukaji wa maadili dhidi ya Kiongozi huyo wa mpira wa miguu nchini.

Taarifa iliyotolewa na TFF, imeeleza kuwa Sekretarieti ya Shirikisho hilo tayari imefungua shauri mbele ya Kamati ya Maadili dhidi ya Haji Manara kutokana na vitendo vya ukiukaji wa maadili.

“Kamati ya Maadili kupitia kwa Mwenyekiti wake tayari imepewa taarifa kuhusu malalamiko dhidi ya Manara, hivyo itapanga siku ya kusikiliza shauri hilo na Mlalamikiwa atapewa taarifa”, imeeleza taarifa.

Hata hivyo, TFF inawakumbusha wanafamilia ya mpira wa miguu kuwa wanabanwa na Katiba na Kanuni mbalimbali za mchezo huo, hivyo wanatakiwa kuwa makini kwa vitendo na kauli zao kuhusu mpira wa miguu.




Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini