KAMATI YA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA MIRABAHA YAZINDULIWA | ZamotoHabari


Na.Khadija Seif, Michuzi Tv


NAIBU Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul amezindua rasmi Kamati maalum ya kushughulikia malalamiko ya wasanii na wadau mbalimbali wa sanaa kuhusu mgao wa Mirabaha kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Taasisi ya Hakimiliki nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, Naibu Waziri Pauline Gekul amesema serikali imejipanga vyema katika kushughulikia chagamoto za malalamiko ya wasanii kwa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (Cosota), kwa kuunda kamati hiyo yenye mkusanyiko wa wadau muhimu.

Naibu Waziri Gekul amesema Waziri Mchengerwa anategemea kamati hiyo itapendekeza mifumo bora zaidi ya kukusanya na kugawa mirabaha inayoshabihiana na mifumo inayotumika kwengineko duniani, kupendekeza njia bora zaidi ya kupambaa na uharamia wa kazi za wasanii pamoja na kupendekeza mifumo bora zaidi ya utendaji wa Taasisi ya Hakimiliki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini, Victor Tesha amesema wataweka nguvu yao yote usiku na mchana kadri wawezavyo kusapoti nguvu kubwa katika kuboresha ufanisi.

"Naomba kutoa ahadi kwamba mimi na wenzangu wote tulioteuliwa tutafanya kazi kwa weledi na ubunifu mkubwa ili kuhakikisha namna bora ya uratibu wa hakimiliki na maslahi ya serikali na wasanii yanatimia, tutahakikisa tunapokea maoni ya kila mdau na kufanya vikao na wote na kuishauri serikali kwa kadri inavyowezekana."


Naibu Waziri Pauline Gekul akizungumza na kamati maalum Jijini Dar es salaam, iliyozinduliwa rasmi Kwa ajili ya kushughulikia Malalamiko ya Mirabaha Kwa Wasanii nchini


Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini Victor Tesha akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kuzinduliwa kwa Kamati hiyo iliyopewa majukumu ya kuhakikisha inafanya utafiti wa namna gani wasanii watalipwa Mirabaha yao bila upendeleo pamoja na kukusanya Malalamiko yao


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini