KIDUNDA NA KATOMPA KUJAZA UWANJA WA MAJIMAJI KESHO | ZamotoHabari

  Na Khadija Seif, Michuzi TV 

MABONDIA wawili Seleman Kidunda na Erick Tshimanga Katompa wamepima uzito na kutarajiwa kupanda ulingoni kuwania ubingwa WBF  katika pambano litakalopigwa  kwenye Uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma.

 Mabondia hao wamepima uzito katika eneo  stendi ya daladala ya Mfananyaki iliopo mjini Songea ambapo pambano hilo  linasubiriwa kwa hamu sambamba na Karim Mandonga anayetarajia kupanda ulingoni dhidi ya Shabani Kaoneka ambao watacheza pambano la utangulizi.

Kidunda na Katompa watapanda ulingoni katika pambano hilo ambalo litapigwa kwa raundi kumi kwenye uzani wa Super middle.

 Mabondia hao mara baada ya kupima uzito kila mmoja amemtambia mwenza akidai atahakikisha anaibuka na ushindi katika pambano.

 Kidunda ameeleza kuwa ataleta ushindi nyumbani mashabiki waondoe hofu.

 “Watanzania nipo vizuri na sina presha ninachotaka kuwaambia ni kwamba nitampiga kwa sababu hao Wakongo wamezoea kuongea halafu hayo mimi siyawezi, njooni kwa wingi Majimaji muone burudani,”.

 Kwa upande wa Katompa amewashukuru wakazi wa mjini wa Songea  kwa mapokezi ambayo ameyapokea huku akiahidi kuonyesha mchezo mzuri katika pambano hilo.
Wapinzani wawili kati ya Bondia wa Ngumi za kulipwa kati ya Selemani Kidunda na Erick Katompa kutoka Kongo wakitunishana misuli mara baada ya kupima uzito uliokamilika kilo 76 Kwa pande zote mbili
Bondia wa Ngumi za kulipwa Karim Mandonga akipima uzito kuelekea pambano la payback dhidi ya mpinzani wake Shaban Kaoneka litakalopigwa uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma.
Shangwe la Wakazi wa Songea mara baada ya kuingia kwa Bondia Selemani Kidunda katika zoezi la upimaji uzito lililofanyika katika stendi kuu ya mabasi ya Mfananyaki Songea Mkoani Ruvuma




Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini