Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
KAMPUNI ya Azam tv imeahidi kuendelea kuwapa burudani bandika bandua watazamaji wao ikiwa ni sehemu ya kuungana Mkono Kampeni ya "sio utani.
Akizungumza na waandishi wahabari Afisa mwendeshaji wa Mkuu kutoka Azam tv Loth Mziray ,wakati wakukaribisha na kutambulisha vipindi vinavyorushwa na Azam tv kusindikiza kampeni ya "Azam tv sio utani" amesema kupitia Azam tv imewapa fursa wasanii na watu mbalimbali kuonyesha uwezo wao na wamekua mkombozi na kuruhusu watu kutafuta kipato cha halali Kwa kutumia vipaji vyao.
"Kupitia Kampeni yetu "Azam tv sio utani" imesheheni vitu mbalimbali ikiwemo Tamthilia za kibongo pamoja na Tamthilia zilizotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ikiambatana na Michezo mbalimbali mpira wa miguu pamoja na masumbwi".
Hata hivyo Mziray amesema Kwa kutambua mchango wa wadau wa Azam tv wameamua kushusha bei ya king'amuzi hicho Ili Kampeni hiyo iweze kuwafikia watu wote nchini na kuburudika na burudani bandika bandua.
"Pambano la Mfaume Mfaume wote wangetamani kushuhudia mapafu ya mbwa akimchakaza mpinzani wake Abdulmonen hivyo Ili burudani iwafikie watu wote tumeona tushushe bei ya king'amuzi kufikia laki Moja ya Kitanzania pamoja na kujiandaa na Fainali ya shirikisho la kombe la Azam litakalofanyika Mkoa wa Arusha ikihusisha yanga fc na costal union kutoka Mkoa wa Tanga hivyo wapenzi wa Azam tv watashuhudia Soka birihani la aina yake.
Kwa upande wake Mtunzi wa Tamthilia inayofanya vizuri Kwa Sasa "Kombolela" Abdul usangi amesema anafurahishwa sana wadau jinsi walivyoipokea Tamthilia hiyo na kuonyesha ni kweli inasadifu maishaa halisi ya baadhi ya familia za Kitanzania Kwa jinsi wanavyoishi.
"Mapokezi ya mama kimbo yalikua makubwa lakini ya Kombolela ni makubwa zaidi nafarijika kuona napata maoni mbalimbali kuwa wanachokiona kinagusa maisha ya watu hivyo silazi damu ikiisha Kombolela maktaba yangu ipo vizuri nashusha kitu kingine kizuri zaidi".
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments