TIMU ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imejiweka pazuri kufuzu hatua ya pili ya mchujo ya kuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN) baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Somalia, kwenye uwanja wa Banjamin Mkapa.
Taifa Stars imepata ushindi huo kupitia kwa Mshambuliaji wake, Abdul Suleiman ‘Sopu’ aliyefunga bao kwa Kichwa kwenye dakika ya 47 ya mchezo, akipokea ‘Krosi’ safi ya Mlinzi wa pembeni, Kibwana Shomari dakika chache baada ya kurejea kwenye mapumziko.
Kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza, Timu ya taifa ya Somalia walikuwa nyumbani Benjamin Mkapa, Kikanuni kutokana na sababu za kiusalama nyumbani kwao. Mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Julai 30, 2022 ambapo Taifa Stars itakuwa nyumbani kwenye uwanja huo huo wa Mkapa.
Taifa Stars inatakiwa kupata sare yoyote au ushindi ili kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kufuzu Michuano hiyo ya CHAN.
Mshindi wa jumla wa mchezo huo kati ya Taifa Stars dhidi ya Somalia atacheza na timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) ambao utakuwa mchujo wa mwisho ‘Play Off’ ya kuwania kufuzu Michuano ya CHAN ambayo itafanyika nchini Algeria, kuanzia Januari hadi Februari, 2023.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments