WASANII WAITWA KUSHIRIKI KUTOA MAONI YA HAKIMILIKI | ZamotoHabari


Na Khadija Seif, Michuzi Tv.


KAMATI ya kuratubu na kusimamia hakimiliki kwa wasanii inatarajia kupokea maoni ya mirabaha kwa wadau mbalimbali wa sanaa za muziki nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini Victor Tesha ametolea ufafanuzi wa Kamati hiyo ilovyojipanga tangu kuteuliwa ndani ya siku 7 na wamejipanga kuwafikia wadau wote nchini na kukusanya Malalamiko na maoni yao namna gani njia Bora zitaweza kutumika kufikwa Kwa Hakimiliki Kwa Wasanii nchini.

Aidha,Tesha ameeleza kuwa Kamati hiyo yenye wabobezi katika tasnia ya Sanaa mbalimbali na rasmi Ukusanyaji huo utafanyika Julai 19 mwaka huu kwa mikoa tofauti ikiwemo Mbeya, Mwanza na Dodoma na Dar es salaam.

Hata hivyo Mwenyekiti anefafanua zaidi kuwa Kamati hiyo itapokea maoni hayo Kwa njia mbili ambapo njia ya kwanza itahusisha njia ya teknolojia na itawawezesha wadau wa Sanaa kutuma maoni kwenye madodoso Mitandaoni pamoja na njia ya mkutano wa ana Kwa ana Kwa Kila mikoa watafika wanakamati kuzungumza na wadau wa Sanaa.

" Hatua hii ya kukusanya maoni kwa wadau itafanyika katika kanda sita kuu zikiwemo Nyanda za Juu, Kanda ya Kati na Kanda ya mashiriki, Kanda ya kaskazini hivyo napenda kuwakaribisha wadau na wasanii Kwa ujumla kushiriki kutoa maoni kwa namn Bora ambayo Kamati itapokea maoni ya kupata mchakato wa kutoa Mirabaha Kwa Wasanii bila upendeleo."

Aidha, Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa Kwa Wasanii ambao umri umeshaenda na ambao Wana Matatizo ya kiafya wataweza kufikiwa na Kamati itapokea maoni yao ikiwa ni sehemu ya kuheshimu mchango wao katika tasnia ya Sanaa nchini.

"Tutaanza rasmi kukusanya maoni Julai 19 mwaka huu na kumalizia Jijini Dar es Salaam Julai 21 mwaka huu, pia tunaenda kufanya mabadiliko na historia inaenda kufanyika katika masuala ya muziki na filamu pamoja tasnia ya Sanaa Kwa ujumla nchini watanzania wawe na imani na sisi ".

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Doren Sinare amesema utoaji wa mirabaha utaendelea kufanyika mwezi huu licha ya kuwepo kwa kamati ya kukusanya maoni ya hakimiliki kwa wasanii.

"Utaratibu wa utoaji wa mirabaha utaendelea kama kawaida licha ya kuwekwa kwa kamati ya hakimiliki tarehe rasmi itatajwa, hivyo wadau watambue kama hii itaendelea na kazi yake kama kawaida."

Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini Victor Tesha akizungumza na waandishi wa habari na kuhimiza wadau wa Sanaa mbalimbali nchini kujitokeza Kwa wingi kushiriki Mikutano iliyoandaliwa Kwa ajili ya kukusanya maoni ya namna ya kugawa Mirabaha Kwa wasanii


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini