FAINALI YA BEST COMEDY CHALLENGE MUBASHARA STBONGO | ZamotoHabari


Na.Khadija Seif, Michuzi Tv


MCHEKESHAJI bora wa wima ( standup comedy) anatarajiwa kuondoka na gari aina ya Toyota crown kwenye fainali ya "the best comedy challenge" usiku wa Agosti 25,2022 katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Jaji mkuu ambae pia ni mchekeshaji maarufu nchini Coy Mzungu amesema ni wakati wa kuipa heshima na hadhi tasnia ya Sanaa hususani katika sekta mahususi ya uchekeshaji nchini.

"Kwa mara ya kwanza tasnia ya uchekeshaji kwa kushirikiana na Startimes wanaenda kumpa thamani mchekeshaji bora atakaepatikana katika Shindano hilo ambalo limedumu wiki 5".

Mzungu akaongeza kuwa gari atakayopatiwa Mshindi itaenda kubadilisha tasnia hiyo na kuona kuwa ni sehemu ya vijana kuwekeza nguvu katika kufanya tasnia ya uchekeshaji kuwa kama tasnia zingine ambazo zinaingiza ajira kwa vijana kwa wingi kupitia vipaji vyao wenyewe.

Coy ameeleza kuwa Shindano hilo lilibeba vijana 20 ambao ni mahiri kwa uchekeshaji lakini kutokana na mchujo uliokua ukifanyika imeweza kubakisha wachekeshaji watano ambao wataweza kupambania gari hiyo aina ya Toyota crown ambayo imetolewa na wadhamini Startimes katika kuhakikisha tasnia ya uchekeshaji inapewa thamani zaidi.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya startimes limited David Malisa amesema Fainali hiyo itafanyika katika ukumbi wa Mlimani city na walio mbali wataweza kupata fursa ya kuona kupitia ving'amuzi vya Startimes kupitia chaneli ya stbongo.

Hata hivyo ameeka wazi kuwa watakaofika ukumbini hapo watapata burudani Kwa mkali wa sugar sugar Jaymelody Huku watavunjwa mbavu na wachekeshaji hao waliofanikiwa kuingia 5 bora ikiwa ni sehemu ya kusaka kura za mwisho mwisho.

Pia ametoa rai kwa watumiaji wa Startimes kulipia vifurushi vyao mapema na kwa watakaolipia kifurushi wataweza kupata nafasi ya kupandishwa kifurushi cha juu yake.

Jaji Mkuu katika Shindano la "The best comedy challenge" Coy Mzungu akiwa pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya startimes David Malisa wakati akizungumza na waandishi wahabari Kwa namna jinsi Mshindi atavyoibuka na gari aina ya Toyota crown mpya huku washindi wengine wanne kuzawadiwa vifuta jasho


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini