GF Trucks & Equipment LTD yaidhamini Timu ya Polisi Zanzibar kwa kuipatia vifaa vya Michezo | ZamotoHabari

Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv Zanzibar
GF Trucks & Equipment LTD yaidhamini Timu ya Polisi Zanzibar kwa kuipatia vifaa vya Michezo ambavyo ni Jezi na soksi ikiwa ni sehemu ya kusapoti sekta ya michezo katika Visiwa Zanzibar.

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Biashara na Masoko Salman Karmali. Amesema vifaa hivyo ni sehemu ya kusherekea miaka 15 ya kibiashara kuunga mkono juhudi za Serikali Zanzibar na hii sehemu kufungua milango ya biashara kwa Visiwa vya Zanzibar.

Ameongeza kuwa GF Truck itaendelea kuangalia kwa namna gani inaweza kuipa nguvu michezo visiwani humo.

"Natoa pongezi kubwa kwa Jeshi la Polisi kuwa sehemu kubwa ya Wadau wa Michezo ikiwa sisi GF Trucks & Equipment LTD tumekuwa sehemu kubwa ya Michezo kule bara na sasa tumekuja kuweka nguvu huku kisiwani. Ndani ya miaka 15 tunayosherekea leo GF Truck tumeweza kushirikiana na timu kadhaa Mbao FC,DTB na sasa Singida big stars inayoshiriki Ligi kuu hii inatupa matumaini kuendelea kutoa support kwenye sekta ya michezo" Amesema

Ameweka wazi kuwa kupitia kampeni ya Royal tour na Uchumi wa bluu wao kama wadau wa Maendeleo wanampongeza sana Mhe Raisi Dkt Mwinyi na viongozi wengine hapa Zanzibar katika hamasa na maendeleo haya.

"Sisi ni wadau wakubwa wa sekta ya maendeleo ya ujenzi,miundombinu na Ujenzi tuna amini kufungua milango ya kibiashara kwa Zanzibar kupitia makampuni ya Ujenzi, wakandarasi na wachimbaji kupitia brand zetu mbili FAW Magari makubwa na XCMG Machine kama excavator. " Amesema

Pia ametoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri na hongera kwa kushiriki sekta ya Michezo.Alimaliza kwa kusema kwa pamoja tukashiriki kwenye SENSA ambayo itafanyika Agosti 23 kwa maendeleo ya nchi yetu.

Kwa upande wa Kamishana wa Jeshi la Polisi CP Hamad Khamis Hamad alipokea vifaa hivyo na kushukuru GF Trucks kwa Udhamini huo na kuhaidi kuwa tayari kushikiriana na GF Trucks watakapo fungua tawi Zanzibar.
Mkurugenzi wa Biashara na Masoko Salman Karmali akiakabidhi Vifaa vya Michezo kwa Kamishana wa Jeshi la Polisi CP Hamad Khamis Hamad.
Mkurugenzi wa Biashara na Masoko Salman Karmali akiagana na Kamishana wa Jeshi la Polisi CP Hamad Khamis Hamad.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini