Kamanda Kova mgeni rasmi uzinduzi mtandao wa Wasanii wanawake | ZamotoHabari

Na Mwandishi Wetu
ALIYEKUWA Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam Suleimani Kova anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mtandao wa Wasanii wanawake Tanzania 'Ladies Faaa' unaotarajia kufanyika Agosti 19 chuoni Splendid Ilala jijini humo.

Akizungumza jana, Katibu wa mtandao huo Asha Salvador alisema uzinduzi huo utasindikizwa na burudani kutoka kundi la Safi.

Salvador alisema uzinduzi huo utahudhuriwa na wadau zaidi ya 80 ambao wataunganisha nguvu ya pamoja itakayosaidia maendeleo.

Aidha Salvador alitumia fursa hiyo kuifafanua taasisi hiyo inayopinga unyanyasaji wa kijinsia kwa vijana wa kike na kiume sambamba na akina mama, elimu itakayotolewa mashuleni na mtaani.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Wasanii wanawake, Anifa Taalib
Katibu wa mtandao wa Wasanii wanawake, Asha Salvador

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini