KANALI JOSEPH BAKARI ATUNUKIWA NISHANI JESHI LA SHIRIKISHO URUSI KWA MCHANGO WAKE KATIKA MICHEZO | ZamotoHabari



  

Naibu waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Shirikisho la Urusi Jenerali Nikolay Pankov akimtunukia nishani Kanali Joseph Bakari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania nchini Urusi Kwa Mchango wake na juhudi zake katika Michezo ikiwemo ya Maofisa wanafunzi yaliyofanyika nchini humo.



WIZARA ya Ulinzi ya Jeshi la Shirikisho Urusi limemtunukia nishani Kwa kuimarisha ushirikiano katika Majeshi Kimataifa Kanali Joseph Bakari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania nchini Urusi.

Kanali Bakari ambaye Ni Mkurugenzi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani ( CISM ) alitunukiwa Nishani hiyo kutokana na mchango wake na juhudi zake katika kusimamia maandalizi ya Michezo ikiwemo ya Maofisa wanafunzi yaliyoafanyika nchini humo hivi karibuni.

Mashindano hayo yaliandaliwa kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya nchi ya Urusi na Ukraine, na yalikabiliwa na changamoto kwa baadhi ya Wanachama walitaka michezo hiyo isifanyike. Kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 2019 hadi 2022.

Nishani hiyo alivishwa na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Shirikisho la Urusi Jenerali Nikolay Pankov mbele ya viongozi mbalimbali wa Jeshi la Shirikisho la Urusi pamoja na wageni wengine wakiwemo washiriki kutoka nchi 20.

Kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Ulinzi ya Shirikisho la Urusi, Nishani hiyo
hutunukiwa kwa Wanajeshi wa Jeshi la Shirikisho la Urusi au Raia kutokana na mafanikio yao katika kuunda na kutekeleza sera ya nchi katika eneo la mahusiano na mashirikiano ya Kijeshi Kimataifa ( international military cooperation).

Aidha, nishani hiyo pia hutunukiwa wananchi wa Shirikisho la Urusi na mashirikisho ya Kimataifa na raia wa nchi nyingine ambao wamechangia kutekeleza kwa mafanikio jukumu maalum la Jeshi la Shirikisho la Urusi Kimataifa.

Pamoja na Kanali Bakari wengine waliotunukiwa Nishani ni Meja Jenerali Maikano Abdullahi kutoka Nigeria ambaye ni Rais wa Baraza la Michezo ya Majeshi barani Afrika na Ndugu Mitryshin Alexei kutoka Urusi ambaye ni Rais wa Shirikisho la mchezo wa Rugby nchini Russia.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini