M-BET Tanzania yafurahishwa na tamasha la Simba Day | ZamotoHabari

 

Na Mwandishi wetu


Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-BET Tanzania imevutiwa na kufana kwa tamasha la klabu ya Simba (Simba Day) ambalo lilifanyika Jumatatu (Agosti 8, 2022) kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mbali ya utambulisho wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujalo wa ligi kuu ya Tanzania Bara, kombe la Azam Federation na Ligi ya mabingwa Afrika, tamasha hili pia ni sehemu ya kusheherekea siku ya kuanzishwa kwa klabu hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko wa M-BET, Allen Mushi alisema kuwa wamefarijika jinsi tamasha hilo lilivyoandaliwa na kufanyika kwake kiasi cha mashabiki kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa ambao uningiza jumla ya watu 60,000.

Mushi alisema kuwa M-BET ilikuwa inajumuika kwa mara ya kwanza tangu kuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo na jinsi mambo yalivyoendeshwa yalikuwa yenye ueledi wa hali ya juu, japo katika kila jambo lazima kutakuwa na mapungufu.


“Ukiachana na changamoto mbalimbali, tamasha lilikuwa la kufana sana, mashabiki wengi walifiki na mbali ya kushuhudia timu hiyo ilishinda mabao 2-0, burudani za wasanii mbalimbali ziliwaburudisha mashabiki hao ambao walianza kuingia uwanjani kuanzia saa 2.00 asubuhi,” alisema Mushi.

M-BET Tanzania imesaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Simba wenye thamani ya Sh bilioni 26.1 na kuwa wadhamini wakuu wa klabu hiyo.

Udhamini huo unaiifanya klabu ya Simba kuwa na thamani kubwa kuliko zote nchini kutokana na kiasi kikubwa cha fedha. Mwaka wa kwanza wa mkataba wao, M-BET wataipa Simba sh4,670,000,000 ambapo kiasi hicho kitaongezeka msimu wa pili ambapo Simba itapata sh4.9 bilioni na mwaka wa tatu wataipa Simba Sh bilioni 5.2

M-BET itazidi kuiongezea Simba fedha kwani mwaka wanne wataipa Sh5.5 billionina mwaka wa tano kiasi cha sh5.8 bilioni itapewa Simba.



Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kufunga bao dhidi ya timu ya St George ya Ethiopia kwenue uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 8, 2022 wakati wa tamasha la Simba Day



Kikosi cha klabu ya Simba katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya St George ya Ethiopia. Klabu ya Simba imedhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-BET Tanzania.



Mashabiki wa klabu ya Simba wakishangilia wakati wa tamasha la Simba Day ambapo mdhamini mkuu wa klabu hiyo, kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-BET Tanzania ilishiriki kwa mara ya kwanza.



wachezaji wa klabu ya Simba na St George wakiingia uwanjani.



Wanachama na mashabiki wa Simba walivyoujaza uwanja wakati wa tamasha la Simba Day ambapo mdhamini mkuu wa klabu hiyo, kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-BET Tanzania ilishiriki kwa mara ya kwanza.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini