Bondia wa Ngumi za kulipwa kutoka Mkoani Morogoro, Karim Mandonga amewataja Mabondia wa kulipwa ambao hatoweza kupigana nao hata angepewa kiasi gani cha fedha, Mandonga amedai Mabondia hao wapo upande wa timu yake.
Mandonga amewataja Mabondia hao ni Twaha Kassim (Kiduku), Selemani Kidunda na Mfaume Mfaume, amesema hapa nchini anaweza kupigana na Bondia yoyote atakayejitokeza.
“Bondia hupaswi kuchagua mtu wa kupigana naye, hiyo ni kazi ya Promota wa pambano, Bondia ukipewa Mpinzani yeyote unapaswa kupigana naye”, amesema Mandonga.
“Mabondia wa nje ya nchi, siwezi kupigana nao ni Mike Tyson na Floyd Mayweather, lakini wengine wote nacheza nao”, ameeleza.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments