Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa kulia akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jacob Mkunda kushoto akiwa Mwenyekiti wa Klabu ya lugalo gofu Michael Luwongo wakimkabidhi zawadi ya Kikombe, Mipira na Begi kubwa la kuhifadhia vifaa mbalimbali vya mchezo wa Gofu mshindi wa Jumla wa shindano la "NBC Patron Trophy 2022" Koplo.William Mtweve wa Lugalo Gofu Klabu katika sherehe za Ufungaji wa Shindano hilo lililofanyika katika Klabu ya lugalo gofu Jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jacob Mkunda, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Venance Salvatory Mabeyo ,Muasisi wa Klabu ya lugalo gofu George Waitara pamoja na Mwenyekiti wa Klabu hiyo brigedia Mstaafu Michael Luwongo mara baada ya kumalizika kwa hafla ya Shindano la (NBC LUGALO PATRON TROPHY 2022) lililoandaliwa mahususi kukaribisha na kuaga Mlezi wa Klabu hiyo lililofanyika jijini Dar es salaam.
Na Khadija Seif, Michuzi Tv
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa serikali itaendelea kumuenzi Jenerali mstaafu Venance Mabeyo kutokana na mchango wake wakukuza tasnia ya michezo nchini.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kufunga Shindano maalum (NBC LUGALO TROPHY 2022) la kumuaga aliyekuwa mlezi wa klabu ya gofu ya Lugalo Venance Mabeyo na kumkaribisha mlezi mpya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda amesema kuwa wizara inampa pongezi nyingi Mabeyo kwa kipindi chote alichokuwa madarakani na kuchochea Wana Michezo kufanya vizuri na kututoa kimasomaso katika Michuano ya umoja wa Madola yaliyomalizika nchini Marekani.
"Serikali inakili kuwa juhudi za Mabeyo zimechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kwa medali 3 zilizokuja nchini kutokea nchini Marekani kwa wanamichezo kutoka jeshini kufuzu Mashindano ya jumuiya ya Madola Marekani ni wazi hamasa yake Kwa wanamichezo jeshini imepelekea ushindi huu ambao kwa Miaka mingi tulikua tunaenda kusindikiza wenzetu lakini kwa mwaka huu tumekua washindi".
Aidha, Mchengerwa amepongeza Jenerali mstaafu George Waitara kwa kuanzisha klabu hiyo na wengine kuiendeleza huku akimkaribisha Mkuu wa Majeshi Jacob Mkunda.
"Namfahamu umahiri wake Mkunda katika Michezo na kwa uzoefu alionao wa kulea vikundi vya michezo ataendeleza yale ambayo waasisi wameacha na kukamilisha mradi wa uwanja wa gofu mkoani Dodoma.
Kwa upande wake Mabeyo aliwashukuru wanachama wa klabu hiyo kwa ushirikiano waliomuonesha tangu alivyopewa ulezi mwaka 2017 na kuwataka kumpa ushirikiano Jenerali Mkunda
"Tumeanzisha klabu nyingine ya gofu Ihumwa kule Dodoma na inaendelea na matengenezo na hivi karibuni itakamilisha mashimo tisa na kumkabidhi Jenerali Mkunda kuhakikisha anaiendeleza ili watu waendelee kucheza gofu".
Pia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda ameahidi kuiendeleza Klabu hiyo ya Golf Nchini sambamba na Klabu mpya ya golf ya JWTZ ihumwa Dodoma.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amempongeza sana Mlezi mstaafu wa Klabu hiyo na kumkaribisha Mlezi mpya huku akihaidi ushirikiano na ushindi kila Mashindano yanayofanyika nje na ndani ya Klabu.
Huku akiwasihi wadhamini kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika mchezo wa gofu na kueka jitihada kuhakikisha watoto (Jr) wanafika mbalimbali Kwa kushiriki Mashindano yanayoandaliwa na wadhamini kama walivofanya benki ya biashara (NBC).
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments