Mchengerwa, Mgeni rasmi Fainali za Pooltable Taifa | ZamotoHabari

WAZIRI wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Omary Mchengerwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi fainali za mashindano ya mchezo wa Pooltable Taifa yanayotarajiwa kufanyika Agosti 19 – 20,mwaka huu katika Uwanja wa ndani wa Benjamini Mkapa(Benjamini Mkapa Indoor National Stadium).

Akizungumza na Mwandishi wetu, Mratibu wa Mashindano hayo wakati wa fainali za mwisho za mikoa ya Morogoro na mkoa wa kimichezo wa Temeke, Michael Machela alisema tayari Chama cha Pool Taifa(TAPA) kimeshampelekea na amethibitisha kuhudhuria fainali hizo zitakazoshilikisha mikoa nane ya kimichezo.

Machela aliitaja mikoa shiriki katika fainali hizo kuwa ni Dodoma ikiwakilishwa na Dodoma Combine, Mbeya ikiwakilishwa na Mbeya Combine, Manyara ikiwakilishwa na Manyara Combine, Iringa ikiwakilishwa na Iringa Combine, Morogoro ikiwakilishwa na timu za Shani Cenema na Blue Room 95, Mkoa wa kimichezo wa Ilala ukiwakilishwa na timu mbili ambazo ni Y2K ya Bugurunu na Fuoni kutoka Zanzibar, Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni ukiwakilishwa na timu mbili ambazo ni Snipers ya Mwenge Mpakani na Tiptop ya Manzese na wenyeji wa fainali hizo Mkoa wa Kimichezo wa Temeke wakiwakilishwa timu mbili ambazo ni Lovingtoni ya Sokota na Mhina timu ya Mtongani kwa Azizi Ally.

Alisema Machela, Fainali hizo zitahusisha timu za wanaume kutoka kila Mkoa lakini pia patakuwa na uchezaji wa mtu mmoja mmoja(Singles) kwa Wanaume na Wanawake.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Isach Togocho alisema tunashukuru mashindano ngazi za mikoa yamekwenda vizuri pamoja na kuwa na changamoto za kifedha zinazowakabili kwani mchezo huo hauna Wadau wa kuudhamini kwa sasa lakini maandalizi yanakwenda vizuri na fainali zitafanyika vizuri pale taifa na kwa kishindo.

Togocho pia aliwashukuru viongozi wa mikoa kwakumaliza vyema mashindano hayo katika ngazi za mikoa na kuwaomba tuendelee kushikamana katika hatua ya fainali za kitaifa pale jijini Dar es Salaam uwanja wa ndani wa Benjamini Mkapa.

Mwisho Togocho alitoa wito kwa Wadau na Makampuni mbalimbali kutoa sapoti ya udhamini wa fainali hizo na mchezo wa Pooltable zinazotarajiwa kuhitimishwa Agosti 20 mwaka huu.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini