Na Zainabu Hamisi,
YALE maonyesho makubwa ya 15 International Afrika Expo Festival Tubingen 2022,Ujerumani, yanatalajiwa kuanza mwanzoni mwa September 1 hadi 04 September 2022 katika viwanja vya maonyesho Fest Platz mjini Tuebingen, nchini Ujerumani.
Wasanii na wajasiliamali mbalimbali kutoka nchini Tanzania ndio wanaongoza kwa wingi katika kushiriki maonyesho hayo makubwa ya Kiafrika barani ulaya.
Mojawapo wa watakao nogesha maoyesho hayo ni mwanamitindo mbunifu wa mitindo rafiki wa mazingira Bi DIANA JOHN MAGESA ambaye mara nyingi amewahai kuipeperusha bendera ya Tanzania katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week, African Fashion Week Canada, UNESCO chini Ufaransa.
Wasanii wa sanaa za maonyesho na wajasiriamali mbalimbali kutoka moja kwamoja nchi Tanzania wanatarajia kuonyesha kazi zao katika maonyesho hayo nchini Ujerumani. KARIBUNI UJERUMANI
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments