Tamasha la SensaBika ni Burudani mwanzo mwisho, Benki ya CRDB yalinogesha | ZamotoHabari

Kuelekea Tamasha kubwa la kuhasisha wananchi kuhesabiwa kwenye Sensa 2022 linalofahamika kama #SensaBika, mapema leo asubuhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Hassan Abbas aliongoza matembezi ya kujiweka mwili sawa kutoka uwanja wa farasi, Oysterbay kuelekea Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es salaam. Tamasha hilo linaendea hivi sasa viwanjani hapo kwa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali nchini.
Sehemu ya vijana wa hamasa wakiongoza matembezi hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Hassan Abbas akiongoza matembezi hayo sambamba na Mmoja wa Wasanii wakongwe nchini maarufu kama Mzee ChiloKatibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Hassan Abbas akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki hiyo, Fredrick Nshekanabo wakati wakifanya mazoezi ya viungo kwenye viwanya vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es salaam leo iliwa ni semehemu ya Tamasha la kuhamasisha wananchi kuhesabiwa kwenye Sensa 2022 linalofahamika kama #SensaBika.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB pamoja na viongozi wengine wakichuana vikali kuvuta kamba dhidi Wasanii, katika Tamasha la kuhamisha wananchi kuhesabiwa kwenye Sensa 2022 linalofahamika kama #SensaBika, linaloendelea hivi sasa kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia alikuwa ni mmoja wa Viongozi walioshiriki kwenye Tamasha hilo.

 






Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini