UMITASHUMTA Yaenda Sambamba na SensaBika | ZamotoHabari


Na Shamimu Nyaki - WUSM

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema wizara hiyo imebuni Kampeni maarufu kwa sasa nchini ya SensaBika ambayo lengo lake ni kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi mwaka huu 2022.

Dkt. Abbasi ameeleza hayo Agosti 04, 2022 Tabora katika Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA ambapo amesema kuwa, wizara hiyo ndio nguvu shawishi ya Taifa pamoja na kutoa furaha kwa watanzania, imeanzisha Kampeni hiyo kutokana na wadau wake wengi kuwa na ushawishi katika jamii ambao wataweza kuhamasisha watanzania kushiriki zoezi la Sensa.
 

''Sisi ni wizara ya kutoa furaha na kupitia sekta zetu tuna wadau wengi ambao
wakitumia Kampeni hii kupitia umaarufu na ushawishi walionao kwenye jamii
itarahisisha kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi kwa jamii kushiriki Sensa.'' Amesema Dkt. Abbasi.

Dkt. Abbasi ametumia nafasi hiyo kumuongoza Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu wa
Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa pamoja na Viongozi, Wanamichezo na Wananchi
waliohudhuria ufunguzi huo kucheza kibwagizo maarufu sana nchini cha SensaBika.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini