Bondia Ibrahim Class kuzichapa na bondia kutoka Mexico Septemba 30, 2022 | ZamotoHabari

Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv
BONDIA kutoka Tanzania Ibrahim Class anataraji kupanda ulingoni kuzichapa na Bondia kutoka Nchini ,Mexico Gustavo Pina Melgar, mpambano utakaopigwa katika ukumbi wa “Next Door” Dar es salaam, tarehe 30 Septemba.

Pambano hili ambalo ndio la kwanza la Lebo ya Mo Boxing Promoshen (au Mo Boxing) inatarajia kuwa fursa kubwa kwa mabondia wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kuweza kufika kileleni na kuwa mstari wa mbele katika ulimwengu wa bondia.

Mohammed Dewji (MO) wa Mo Boxing amesema: tumefurahi kuzindua lebo ya Mo Boxing Promoshen itakayosaidia ndondi za Afrika kwa ujumla. Dhumuni kubwa ni kukuza ndondi za Afrika kwenye jukwaa la kimataifa, kuukuza mchezo wa ndondi na kuifanya Tanzania kuwa kitvu kwa Afrika. Kwa upande wa matukio makuu bondia mtaalamu nchini Ibrahim Class atakuwa ndio kilele dhidi ya Gustavo Pina mwenye ubobefu katika fani hii.

"wakifuatiwa na mapambano kati ya Alfred Lamptey – Namba 1 toka Ghana katika uzito wa WBO bingwa wa dunia kwa vijana na Abraham Ndauendapo uzito wa WBC bingwa wa Fedha wa dunia."

Amesema Wengine wenye vipaji chipukizi ni kama Juma Choki, Jose Hernandez, Nicholas Mwangi na Emmanuel Mwakyembe. Tamasha hili halitavutia tu mashabiki toka Afrika bali litakuwa la kimataifa.

Kwa upande wa ndondi za kawaida tutakuwa na Sultan Al Nuaimi (rekodi: 8-0-0, 5 KO) atakaekutana na Haji Juma Mwalugo (rekodi: 18-18-5, 9 KO), Sameer Anwar (rekodi: 4-1-0, 3 KO) dhidi ya Mustapha Dotto (rekodi: 22-27-6, 10KO), Sadra Mohammed (rekodi: 2-2-0, 0KO) dhidi ya Lulu Kayage (7-8-3, 2KO)Bw Ahmed Saddiq wa Mo Boxing nae amesema: sisi tumekuza ndondi toka chini mpaka ilipo sasa kwa nchi za Falme za Kiarabu (UAE) na Kazakhstan, na sasa lengo letu ni kuipandisha Afrika katika Nyanja za kimataifa.

Mo Boxing Promotion ni muendelezo utakaohusisha vipaji vya kitaifa na kimataifa kote barani Afrika na duniani. Tamasha letu hili la mwezi Septemba limefanikiwa kwa hisani ya wadau tofauti wakiwemo Bajaj Group Tanzania (pikipiki za Boxer) kama wadhamaini wakuu, hoteli ya Whitesands, Kampuni ya Aone kupitia kinywaji cha Mo Xtra na wauzaji wa tiketi Otapp.Hili ni tamasha kubwa kufanyika nchini litakalowapatia mashabiki burudani toka mwanzo hadi mwisho.

Mauzo ya tiketi yatatangazwa karibuni.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini